Polisi nchini Ufaransa wamewakamata watu watatu wanaohusishwa na shambulizi la lori la siku ya Alhamis mjini Nice lililosababisha vifo vya watu 84.
Wale waliouawa walikuwa kati ya umati mkubwa uliokuwa ukitizama maonyesho ya fataki, wakati lori lilivurumishwa makusudi kwenda eneo walikuwa.
Zaidi ya watu 50 wako hali mahututi hospitalini. Siku tatu za maombolezi zimeanza kwa waathiriwa wanaotoka nchi kadha.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni