Kampuni ya
kuzalisha umeme nchini Kenya, KENGEN imetuma taarifa kwa vyombo vya
habari ikiomba radhi kwa ukosefu wa umeme Kwa hapo jana.
Hilo sio jambo geni.
Mara kwa mara umeme hupotea nchini Kenya kwa sababu moja au nyengine, sawa tu na mataifa yote barani Afrika
Hata
hivyo sababu walioitoa KENGEN kwa ukosefu huo wa umeme Kwa takriban saa
nne kote nchini humo ndio imewaacha wengi wamepigwa na butwaa !
Nyani.
Amini usiamini, KENGEN imempata nyani mmoja katika
eneo maalum lenye 'swichi' hiyo katika mtambo wa kuzalisha umeme ulioko
kwenye bwawa kuu la Gitaru Mashariki mwa Kenya.
Sasa kampuni hiyo inasema huenda nyani huyo ndiye aliyezima umeme kote nchini Kenya !
Kengen
inasema kuwa huenda nyani huyo aliangukia mashine hiyo ndogo na
''kusababisha hitilafu ya takriban megawati 180 za umeme ambao ndio
uliosababisha ukosefu wa umeme kote nchini Kenya.''
Kwa takriban saa nne taarifa hiyo ilielezea.