BREAKING NEWS

Jumamosi, 2 Julai 2016

Serengeti boys wasonga mbele



 FT: Shelisheli U17 0-6 Tanzania (Serengeti) U17 ( Agg 0-9 ) - Tanzania sasa wataumana na South Africa katika raundi inayofuata ya kuwania kufuzu kucheza AFCON under 17.







Tetesi za soka Ulaya




Image copyrightEPA
Image captionVan Persie
Henrikh Mkhitaryan, 27, atakamilisha uhamisho kutoka Borussia Dortmund kwenda Manchester United weekend hii.
Image copyrightGETTY
Image captionSaido Berahino
Mchezaji huyo kutoka Armenia atagharimu takriban pauni milioni 26 (Daily Mail), Manchester City wapo tayari kulipa hadi pauni milioni 50 kumsajili beki John Stones, 22, kabla ya kuanza kwa mechi za kabla ya msimu (Telegraph), Crystal Palace wamekubali kulipa pauni milioni 12.5 kumsajili beki wa West Ham James Tomkins, 27 (Daily Mail), mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich wanafikiria kumsajili beki wa kati wa Arsenal, 30, ambaye mkataba wake Emirates unamalizika mwaka 2019 (Evening Standard),
Image copyrightAFP
Image captionAxel Witsel
Everton wamekubali kumsajili kiungo wa Ubelgiji Axel Witsel, 27, kutoka Zenith St Petersburg na watamlipa mchezaji huyo zaidi ya pauni 100,000 kwa wiki (Squawka), Stoke City wametoa dau la pauni milioni 16 kutaka kumsajili mshambuliaji wa West Brom, Saido Berahino, 22, na wako tayari kumlipa pauni 70,000 kwa wiki (Mirror).
Image copyrightALL SPORT
Image captionArsenal
Burnley wanataka kumfanya beki Michael Keane, 23, kuwa mchezaji anayelipwa zaidi katika historia ya klabu hiyo ili kuzuia kusajiliwa na Leicester City (Mirror), mchezaji wa zamani wa Arsenal na Manchester United Robin van Persie, 32, anauzwa na klabu yake ya Fernabahce (Evening Standard), mshambuliaji wa Manchester United Ashley Fletcher, 20, amekataa mkataba mpya na atafanya vipimo West Ham (Manchester Evening News).

Kamishna wa UK kuhusu EU kujiuzulu




Image copyrightGETTY
Image captionLord Hill
Kamishna anayeiwakilisha Uingereza katika muungano wa Ulaya Lord Hill anatarajiwa kujiuzulu akisema kuwa kile kilichofanyika hakiwezi kurudishwa baada ya Uingereza kupiga kura ya kujiondoa katika muungano huo.
Katika taarifa ,amesema kuwa haamini ni sawa kwa yeye kuendelea na kazi yake kama kamishna anayesimamia huduma za fedha.
Lakini ataendelea kuhudumu kwa wiki kadhaa ili ajiuzulu kwa mpangilio.
Akiwa mwandani wa waziri mkuu David Cameron ,Lord Hill amehoji kwa Uingereza kusalia katika muungano wa Ulaya.
Tangazo hilo la Lord Hill linajiri huku waziri wa kwanza wa Uskochi Nicola Sturgeon akisema kuwa ataanzisha mazungumza ya haraka na muungano wa Ulaya ili kuilinda haki ya Uskochi katika muungano huo baada ya Uingereza kujiondoa.

Profesa aliyebeba mtoto mgongoni apata sifa




Image captionProfessor Honore Kahi
Profesa mmoja wa chuo kikuu amesifiwa pakubwa nchini Ivory Coast kwa kumbeba mtoto wa mmoja wa wanafunzi wake mgongoni wakati wa masomo.
Picha za Honore Kahi wa chuo cha Bouake, zimesambaa pakubwa kwenye mitandao ya kijamii.
Alisema aliamua kumsaidia mwanamke katika darasa lake wakati mtoto alianza kulia.
Picha zilizochukuliwa na mwanafunzi mwingine zinamuonyesha, bwana Kahi akifunza huku mtoto akiwa mgongoni.

Balozi wa S Leone atekwa nyara Nigeria




Image captionRamani
Naibu balozi wa Sierra leone nchini Nigeria ametekwa nyara.
Maafisa wa Sierra Leone's wanasema Nelson Williams alitekwa nyara akiwa katika jimbo la Kaduna.
Hata hivyo maafisa wa Nigeria wanasema haijbainika wazi mahali ambapo utekaji huo ulifanyika.
Haijulikani ni akina nani waliomteka nyara balozi huyo, japo wametaka kulipwa kikombozi.

Jeshi la Israel lashambulia Gaza




Image copyrightREUTERS
Image captionGaza
Ndege za kivita za Israeli zimetekeleza msururu wa mashambulzi ya asubuhi mapema huko Gaza.
Jeshi la Israeli linasema limeshambulia maeneo manne yanayohusishwa na wapiganaji wa Hamas ambao wanadhibiti eneo hilo.
Kulingana na taarifa kutoka kwa vyanzo nchini Palestina, watu wawili wameuawa.
Image copyrightREUTERS
Image captionGaza
Awali kombora lililofytuliwa kutoka Gaza liligonga jengo la shule ya chekechea japo halikuwa na watu.

Viongozi 2 wa IS wauawa Mosul, Iraq



  •  
Image captionMosul Iraq
Viongozi wawili wakuu wa kundi la kigaidi la Islamic State waliuawa katika mashambulizi ya angani ya vikosi vya muungano vinavyoongozwa na Marekani, katika mji wa Mosul nchini Afghanistan mwezi ulopita.
Msemaji huyo anasema vikosi vya muungano vimeanza kuwafurusha wapiganaji hao katika eneo la kusini mwa Mosul.
Haya yanajiri baada ya vikosi hivyo kuchukua udhibiti wa mji wa Fallujah kutoka mikononi mwa IS. Shambulizi hilo la angani karibu na mji wa Mosul lilifanyika wiki ilopita.
Image captionMosul Iraq
Mosul ni mji wa pili kwa ukubwa nchini Iraq, na unasemekana kuwa ngome kuu ya islamic state.
Kulingana na Pentagon, makamanda wawili wakuu wa kundi hilo waliuawa akiwemo naibu waziri wa vita Basim Muhammad Ahmad , na kamanda mkuu wa kundi hilo Hatim Talib al-Hamduni.
Kwa sasa inaonekana lengo kuu la vikosi vya Iraq litakuwa kuchukua udhibiti wa mji wa Mosul.
Msemaji wa Pentagon anasema mauaji ya viongozi hao, pamoja na mashambulzi ya angani dhidi ya kundi hilo kwa kipindi cha mwezi mmoja uliopita, yameathiri pakubwa uongozi wa kundi hilo mjini Mosul.
Image copyrightREUTERS
Image captionMosul Iraq
Hii itatoa nafasi bora kwa vikosi vya Iraq kunyakua mji huo, kwa usaidizi wa muungano wa majeshi ya kimataifa.

Mwanamke kujifungua 'mjukuu wake'




Mwanamke ambaye anataka kutumia mayai ya uzazi ya bintinye ili kumzaa mjukuu wake ameshinda kesi mahakanani na kuruhusiwa kufanya hivyo.
Mwanamke huyo wa umri wa miaka 60 alikuwa amekatazwa kupeleka mayai ya bintiye kwenye kliniki moja nchini Marekani hali iliyosababisha akate rufaa.
Bintiye ambaye aliaga dunia mwaka 2011, anaripotiwa kumuambia mamake amzalie watoto wake. Lakini mamake alishindwa katika kesi mwaka uliopita.
Hata hiyo aliruhusiwa kupinga hukumu hiyo katika mahakama ya rufaa mjini London mbele ya jopo la majaji watatu.
Mwaka 2014 halmashauri inayohusika na mayai ya uzazi, ilisema kuwa mayai hayo hayangetolewa mjini London, kwa sababu bintiye hakuwa ametoa idhini kamili kabla ya kifo chake akiwa na umri wa miaka 28.
Lakini kwenye kesi ya sasa mawakili waliawaambia majaji kuwa, mwanamke huyo alikuwa anataka kutimiza matakwa ya bintiye ya kuzaa mtoto akitumia mayai yake na kisha amlee mtoto huyo.

Mwili wa wakili aliyetoweka Kenya wapatikana


  • 6
Image captionKimani
Mili miwili imepatikana nchini Kenya wakati wa usakaji wa wakili mmoja aliyetoweka wiki moja iliopita akiwa na mteja wake na dereva wa taxi.
Awali afisa mkuu wa kitengo cha jinai nchini Kenya Ndegwa Muhoro alinukuliwa na gazeti la Daily Nation akisema kuwa juhudu za kuutafuta mwili wa tatu unaodaiwa kuwa wa mteja wa Bw Kimani ,Josphat Mwenda zinaendelea.
Afisa mkuu wa polisi nchini humo tayari ameagiza kukamatwa kwa maafisa watatu wa polisi wanaoshukiwa kuhusika na utekaji nyara wa wakili Willie Kimani.
Bw Kimani alikuwa akimwakilisha mteja wake aliyekuwa akiwasilisha malalamishi dhidi ya polisi.
Chama cha wanasheria nchini kinaamini kwamba alitekwa nyara baada ya kuondoka mahakamani katika mji mkuu Nairobi.
Duru za polisi zimeambia BBC kwamba mili miwili ilipatikana kandokando ya mto yapata kilomita 70 kaskazini mashariki mwa Nairobi.
Usakaji unaendelea katika eneo hilo ili kuupata mwili mwengine wa tatu kulingana na gazeti la Kenya,The Standard.
Bw Kimani alikuwa akilifanyia kazi shirika moja la hisani kuhusu sheria nchini Marekani, International Justice Mission ambalo huzingatia visa vya maafisa wa polisi wanaotumia vibaya mamlaka yao.

Uganda yavunja mkataba na kampuni ya Urusi




Park Geun-hyeImage copyrightAFP
Image captionPark Geun-hye alizuru Uganda mwezi Mei
Serikali ya Uganda imevunja mkataba wake na kampuni ya Urusi kuhusu mpango wa kujenga kiwanda cha kusafisha mafuta.
Serikali ilikuwa imekamilisha mazungumzo na kampuni hiyo ya Rostec Global Resources Consortium.
Lakini inasema baadaye kampuni hiyo ilianza kuongeza masharti mengine hata baada ya makubaliano ya mwisho kufikiwa.
Mkataba huo sasa umekabidhiwa kampuni ya SK Engineering kutoka Korea Kusini.
Kampuni hiyo iliibuka ya pili katika shughuli ya kutoa zabuni.
Hatua hiyo imejiri wiki chache baada ya Rais wa Korea Kusini Park Geun-hye kuzuru Uganda.

Mtalii afariki akijipiga picha Peru


MachuImage copyright
Image captionWatu milioni moja walizuru Machu Picha mwaka 2014 wakiwa peke yao
Mtalii kutoka nchini Ujerumani amefariki dunia baada ya kuanguka akijipiga picha nchini Peru.
Oliver Park, 51, alianguka kwenye eneo la mabaki ya kale ya Machu Picchu katika milima ya Andes nchini Peru.
Park alipuuza tahadhari za kiusalama na onyo kutoka kwa walinzi na akaenda eneo lisiloruhusiwa watu kujipiga picha.
Taarifa zinasema alienda kujipiga picha eneo la mwamba Jumatano.
Alijaribu kuruka juu ndipo ajipiga picha akiwa hewani lakini akateleza na kutumbukia kwenye bonde.
Maafisa wa uokoaji waliupata mwili wake Alhamisi na kuupeleka kituo cha polisi kilichoko karibu.
Polisi wamesema mwili wake utapelekwa chumba cha kuhifadhia maiti katika mji wa Cusco.

SOMA ZAIDI HAPA