Image copyrightTFF TWITTERImage captionYanga watakutana na Medeama Jumamosi saa kumi jioni
Wapinzani wa klabu ya Young Africans, katika michuano ya kuwania Kombe la Shirikisho Barani Afrika, Medeama kutoka Ghana, wametua Dar es Salaam tayari kwa mechi baina ya timu hizo Jumamosi.
Wachezaji hao waliwasili Dar Alhamisi na wakafanya mazoezi katika uwanja wa Karume.
Yanga itaikaribisha Medeama kwa mchezo wa tatu kuwania taji hilo hatua ya makundi katika uwanja wa taifa Dar es Salaam.
Mchezao huo utaanza saa 10.00 jioni
Michezo miwili ya awali ya Yanga katika michuano hiyo ilikuwa ni dhidi ya Mo Bejaia ya Algeria ambako ilipoteza kwa bao 1-0 kabla ya kupoteza tena dhidi ya TP Mazembe, mechi iliyopigwa jijini Dar es Salaam.
Mchezo wa Jumamosi utachezeshwa na waamuzi kutoka Misri ambao ni Ibrahim Nour El Din atakayekuwa mwamuzi wa kati; akisaidiwa na Ayman Degaish na Samir Gamal Saad wakati mwamuzi wa akiba akiwa ni Mohamed Maarouf Eid Mansour, kwa mujibu wa Shirikisho la Kandanda la Tanzania (TFF)
Image copyrightAFPImage captionHii ni mara ya kwanza kwa Ureno kushinda taji kubwa kama hilo.
Kundi kubwa la mashabiki wa Ureno limeendelea kusheherekea bada ya timu yao ya taifa kuifunga Ufaransa katika michuano ya Euro 2016 mjini Paris.
Ureno imeshinda 1-0 katika muda wa nyongeza na kuwaacha mashabiki wa Ufaransa katika hali ya simanzi ndani ya dimba la Stade de France huku mitaa ya Lisbon ikirindima kwa shangwe kubwa.
Ureno illicheka karibia mda wote bila huduma ya nyota wake Cristiano Ronaldo aliyeumia na kutolewa nje dakika 25 ya mchezo huo na baadaye kurejea na kulinyanyua kombe hilo.
Amesema kombe hilo ni kwa ajili ya Wareno wote pamoja na wote wanaioshabikia timu hiyo mjini Paris.
Hii ni mara ya kwanza kwa Ureno kushinda taji kubwa kama hilo.
Mchezaji nyota wa Argentina na Barcelona Lionel Messi amehukumiwa kifungo cha miezi 21 jela baada ya kupatikana na makosa ya kutumia ulaghai wakati wa ulipaji ushuru, vyombo vya habari nchini Uhispania vinaripoti.
Babake, Jorge Messi, pia amehukumiwa kufungwa jela kwa kuilaghai Uhispania €4.1m (£3.2m; $4.6m) kati ya 2007 na 2009.
Wakati wa kesi, waendesha mashtaka walisema maeneo salama yenye kinga dhidi ya ushuru Belize na Uruguay yaliyumiwa kuficha mapato kutokana na uuzaji wa haki za picha za mchezaji huyo.
Lakini Messi amesema hakufahamu lolote kuhusu masuala yake ya kifedha.
Wawili hao hata hivyo hawatarajiwi kufungwa jela.
Chini ya mfumo wa haki nchini Uhispania, mtu anaweza kutumikia kifungo chochote kilicho chini ya miaka miwili nje ya gereza.
Messi na babake pia wanaweza kukata rufaa katika Mahakama ya Juu nchini humo.
Mwanafunzi mmoja wa chuo kikuu kimoja nchini Kenya amejitia kitanzi baada ya kupoteza dau la shilingi 80,000 sawa na dola $800 aliloweka katika mechi za Euro 2016.
Kwa mujibu wa gazeti moja nchini Daily Nation mwanafunzi huyo alikuwa ameweka dau la dola $ 400 kwa ushindi wa Ujerumani na pesa zingine sawa na hizo kwa ushindi wa Italia.
Image copyrightGETTYImage captionKipa wa ujerumani akiokoa mkwaju wa penalti
Hata hivyo kinyume na matarajio yake mechi hiyo iliishia sare na kumaanisha kuwa alikuwa amepoteza pesa hizo zote.
Alifunga safari kutoka mjini Nairobi hadi kwao magharibi mwa Kenya alipojitia kitanzi nyuma ya nyumba ya mamake mzazi katika kijiji cha Ondome Uriri jimbo la Nyanza.
Afisa mkuu wa polisi katika eneo hilo David Kirui anasema kuwa marehemu aliacha ujumbe akisema hakuona haja ya kuendelea kuishi baada ya kupoteza pesa alizopewa za kulipia karo za chuo kikuu.
Image copyrightREUTERSImage captionUjerumani hata hivyo ilishinda kwa mikwaju ya penalti ilyofuatia.
Ujerumani hata hivyo ilishinda kwa mikwaju ya penalti ilyofuatia.
Ujerumani itachuana dhidi ya wenyeji Ufaransa katika nusu fainali baadaye leo.
Image copyrightAPImage captionMechi hiyo iliishia sare baada ya muda wa kawaida
Mshindi kati yao atachuana dhidi ya Ureno iliyoizaba Wales mabao 2-0 katika mechi ya nusu fainali iliyochezwa jana.
Sasa miapango ya mazishi imeanza huku swala la kuenea kwa michezo ya bahati na sibu ikizua tena mjadala miongoni mwa wapenzi wa kandanda na jamii kwa jumla.
Je kuna njia yeyote ambayo serikali inaweza kuingilia kati ilikuzuia uraibu wa michezo hiyo ya bahati na sibu kugeuka na kuwa karaha ?
Image copyrightAFPImage captionBasi lilowabeba wachezaji wa Iceland likipita mitaani
Maelfu ya raia wa Iceland wamekusanyika katikati ya mji mkuu wa Reykjavik kukaribisha msafara wa timu yao ya taifa kwa mafanikio iliyopata kwenye michuano ya Kombe la mataifa Bingwa barani ulaya mwaka huu 2016.
Wachezaji walipita katikati ya mji wakiwa ndani ya basi kubwa la wazi wakisindikizwa na ngoma hadi katika mlima wa Arnarholl ambapo mashabiki waliwasalimia kwa shangwa na makofi .
Iceland ambayo imeshiriki kwa mara ya kwanza mashindano makubwa ya Kombe la mataifa barani Ulaya ilifikia ukingoni mwa mashindano mwaka huu baada ya kupata kichapo kutoka kwa Ufaransa kwa magoli 5 - 2.
Hata hivyo kabla ya kuondolewa ilionyesha maajabu pale ilipoiondoa England kwenye hatua ya kumi na sita bora.
Mkufunzi Jose Mourinho amesema kuwa yuko tayari kuchukua jukumu la kuifunza Manchester United,akisisitiza ''niko mahala nitakapo''.
Raia huyo wa Ureno mwenye umri wa miaka 53 aliongezea: ''Nadhani ni kazi ambayo kila mtu anahitaji na sio wengi ambao huipata na mimi nimeipata''.
Mkufunzi huyo wa zamani wa Chelsea anachukua mahala pake Louis Van Gaal,ambaye alifutwa kazi baada ya United kushinda kombe la FA mnamo mwezi Mei.
Mourinho anasema kuwa anachukizwa kuona kwamba United haitashiriki katika mechi za kombe la vilabu bingwa Ulaya msimu ujao lakini akasisiiza kuwa yuko Old Trafford kushinda mataji.
''Ni kweli hatuwezi kupata kila kitu ,lakini tunataka''.Alipoulizwa iwapo ana chochote cha kujionyesha baada ya kufutwa kazi akiwa Chelsea,alijibu:''Kuna mameneja ambao hawajashinda mataji kwa kipindi cha miaka 10 iliopita.Wengine bado kabisa.Mara yangu ya mwisho kushinda taji ni mwaka uliopita''.
Mshambuliaji wa England na Tottenham, Harry Kane atasaini mkataba mpya kusalia White Hart Lane wenye thamani ya pauni milioni 5 kwa mwaka wiki hii (Independent), Jose Mourinho ana uhakika wa kumshawishi kiungo kutoka Ufaransa Paul Pogba, 23, kurejea tena Manchester United miaka minne baada ya kuondoka na kwenda Juventus (Daily Mail), Manchester United wapo tayari 'kuvunja benki' ili kumsajili Pogba, huku dau likidhaniwa kufika hadi pauni milioni 100 (Telegraph).
Image copyrightAFPImage captionPogba kurejea OT?
Kiungo wa Paris St-Germain, Blaise Matuidi, 29, amepewa ruhusa ya kuondoka katika kambi ya Euro 2016 ya Ufaransa na kwenda England kwa ajili ya mazungumzo ya kuhamia Manchester United (Goal), Manchester United na Liverpool wote wanataka kumsajili kiungo wa Porto Ruben Neves, 19 (Sun), Manchester City wanakaribia kukamilisha usajili mwingine unaodhaniwa kuwa wa pauni milioni 40 kumchukua winga wa Schalke, Leroy Sane, 20 (Manchester Evening News), Tottenham hatimaye wanakaribia kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa AZ Alkmaar, Vincent Janssen, 21, wiki hii na pia wanataka kumsajili mshambuliaji wa Roma, Antonio Sababria, 20 na Lucas Alario, 20 kutoka River Plate (Daily Mirror).
Image copyrightREUTERSImage captionAlvaro Morata anasakwa na vilabu kadhaa vya EPL
Arsenal wako tayari kumpa Alvaro Morata, 23, mshahara wa pauni 144,000 kwa wiki kumshawishi kuhamia Emirates (Don Balon), Crystal Palace wameongeza dau lao kufikia pauni milioni 31.5 kumtaka mshambuliaji wa Liverpool Christian Benteke, 25, baada ya dau la pauni milioni 25 kukataliwa (Sun), Crystal Palace wanakamilisha uhamisho wa beki wa West Ham James Tomkins, 27 (Evening Standard), Chelsea wanafikiria kutoa pauni milioni 12 kumchukua mshambuliaji wa Southampton Graziano Pelle, 30, iwapo watashindwa kumpata Morata kutoka Real Madrid (Evening Standard).
Image copyrightAFPImage captionRobin van Persie huenda akarejea London
Kiungo wa Liverpool Lucas Leiva, 29, yuko tayari kuhamia Besitkas ya Uturuki (Fanatik), Fernabahce wanataka kumsajili mshambuliaji wa Newcastle Siem de Jong, 27 (Haberturk), West Ham na Crystal Palace ni miongoni mwa timu za EPL ambazo Robin van Persie, 32, ameruhusiwa kwenda na klabu yake ya Fernabahce (Daily Mail), mshambuliaji wa zamani wa Aston Villa Charles N'Zogbia, 29, anajaribu kufufua mpira wake kwa kufanya mazoezi na Sunderland (Birmingham Mail). Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa
# Taarifa Kutoka Ufaransa Zinasema Kuwa Kiungo wa Timu Ya Taifa Ya Ufaransa na Klabu Ya PSG " #BlaiseMatuidi " Ameondoka Kwenye Kambi Ya Timu Yake Ya Taifa Baada ya Ushindi wa Hapo Jana Dhidi Ya Iceland na ameelekea Uingereza Kwaajili Ya Mazungumzo ya Usajili wake na Klabu ya Manchester United ndio Wanaotajwa Kuwania Saini Ya Kiungo huyo , Lakini Pia Chelsea Walikuwa Wanawania Saini Ya Kiungo huyo Tangu Mwakajana ... Wakala wa Ibrahimovic Mino Raiola ndio Wakala wa Matuidi Kwahiyo Huwenda Mchezaji huyo Akawa na Mazungumzo na Man Utd.
Image copyrightGETTYImage captionMichy alifunga dhidi ya Hungary baada ya kuingia nafasi ya Romelu LukakuKlabu ya Chelsea ya Uingereza imemsajili mshambuliaji wa Ubelgiji mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.Michy Batshuayi amehamia Chelsea kutoka klabu ya Marseille ya Ufaransa na kutia saini mkataba wa miaka mitano.
Mamake ni Viviane Leya Iseka na babake Pino Batshuayi.
Michy alikuwa na fursa ya kuchezea timu ya taifa ya DR Congo kutokana na asili ya wazazi wake lakini mwaka jana aliamua kuwa mchezaji wa Ubelgiji.
Image copyrightGETTY
Aliwachezea mechi ya kwanza dhidi ya Cyprus Machi 2015 na kufunga bao.
Michy, 22, ambaye ndiye mchezaji wa kwanza kununuliwa na meneja mpya wa Chelsea Antonio Conte Stamford Bridge, hujulikana kwa jina la utani kama Batsman.
Kakake Aaron Leya Iseka ni mchezaji wa klabu ya Anderlecht ya Ubelgiji.
Chelsea hawakutangaza wazi bei waliyomnunua Michy lakini inaaminika kuwa takriban £33m (euro 40m).
Mshambuliaji huyo, aliyefunga mabao 23 akichezea Marseille msimu uliopita, alifungia Ubelgiji wakati wa ushindi wao hatua ya 16 bora dhidi ya Hungary katika Euro 2016 na pia aliwachezea walipotolewa kwenye michuano hiyo hatua ya robofainali na Wales.
Mabingwa wa Ligi Kuu ya England Leicester City wamekubaliana na CSKA Moscow kumsajili mshambuliaji kutoka Nigeria Ahmed Musa. Hii ni kwa mujibu wa wakala wa mchezaji huyo. Musa, 23, alijiunga na CSKA mwaka 2012 na kupachika mabao 54 katika mechi 168. BBC Sport inasema Leicester 'wamevunja benki' katika ada ya kumsajili mchezaji huyo. BBC Sport pia inasema Musa alikataa kwenda Southampton, Everton na West Ham. Kocha wa CSKA Moscow Leonid Slusky amekiri kuwa Mnigeria huyo ambaye anaweza kucheza kama winga au mshambuliaji wa kati, anaondoka Urusi.
Image copyrightGETTYImage captionManchester United wamewaambia Juventus kuwa wako tayari kulipa pauni milioni 100 kumsajili
Manchester United wamewaambia Juventus kuwa wako tayari kulipa pauni milioni 100 kumsajili kiungo kutoka Ufaransa Paul Pogba, 23, na watampa mshahara wa pauni 250,000 kwa wiki (Mail on Sunday).
Arsenal watampa mkataba mpya Arsene Wenger kwa matumaini ya kumshawishi asiondoke baada ya tetesi kuzagaa kuwa chama cha soka cha England, FA, kinamnyatia (Observer).
Meneja mpya wa Manchester City, Pep Guardiola anataka kumsajili mshambuliaji kutoka Uruguay anayeichezea Barcelona, Luis Suarez, 29, anayedhaniwa kuwa na thamani ya pauni milioni 85, pamoja na kiungo Mjerumani anayechezea Real Madrid, Toni Kroos, 26, ambaye kipengele chake cha uhamisho kina thamani ya pauni milioni 63 (Sunday Mirror).
Mabingwa wa Ufaransa Paris St-Germain wamekubali kumsajili kiungo kutoka Poland anayechezea Sevilla Gregorz Krychowiak, 26, kwa pauni milioni 22 (Marca).
Image copyrightREUTERSImage captionPep Guardiola anataka kumsajili mshambuliaji kutoka Uruguay anayeichezea Barcelona, Luis Suarez, 29
Liverpool watapambana na Everton katika kumsajili kiungo kutoka Ubelgiji Axel Witsel, 27, anayecheza soka Zenith St Petersburg nchini Urusi (Sunday Mirror).
Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United na Arsenal, Robin van Persie, 32, huenda akarejea katika ligi kuu ya England baada ya klabu yake ya sasa Fernabahce ya Uturuki kuwaambia West Ham na Crystal Palace kuwa wanaweza kumsajili (Sun on Sunday).
Chelsea wamefanikiwa juhudi za kumsajili beki kutoka Senegal, Kalidou Koulibaly, 25, anayechezea Napoli kwa pauni milioni 30 (Sunday Mirror).
Image captionTetesi za soka Ulaya- leo Jumapili
Tottenham wanajiandaa kutoa pauni milioni 38, kumtaka mshambuliaji wa Inter Milan, Mauro Icardi, 23, na tayari wamepeleka wawakilishi wao Italy kuzungumza na mchezaji huyo kutoka Argentina (GianlucaDiMarzio), kipa wa Spurs Hugo Lloris, 29, ananyatiwa na Real Madrid kwa pauni milioni 35 (Sunday Mirror).
Meneja wa Tottenham, Mauricio Pochettino yuko tayari kumuuza Ryan Mason, 25, kwenda Hull City iliyopanda daraja kwa pauni milioni 10 (Sun on Sunday), kiungo wa Watford Jose Manuel Jurado, 30, amehusishwa na kuhamia Espanyol na kuungana na meneja wake wa zamani Quique Sanchez Flores (Fichajes).
Image copyrightAFPImage captionFernabahce ya Uturuki wamewaambia West Ham na Crystal Palace kuwa wanaweza kumsajili Robin van Persie.
Middlesbrough watakamilisha usajili wa pauni milioni 11.75 wa kiungo kutoka Atalanta, Marten de Roon, 25, baada ya kukubaliana maslahi binafsi na mkataba wa miaka minne (Gazette),
Timu nne za EPL zimekuwa zikiwasiliana na wawakilishi wa mshambuliaji wa Wales, Hal Robson Kanu tangu alipopachika bao dhidi ya Ubelgiji kwenye michuano ya Euro 2016.
Kanu ni mchezaji huru baada ya kuachiliwa na klabu yake ya Reading (Sky Sports).
Stoke huenda wakalazimika kulipa takriban pauni milioni 20 kama wanataka kumsajili mshambuliaji wa West Brom, Saido Berahino, 22 (Stoke Sentinel).