Rais wa Nigeria
Muhammadu Buhari amekutana na msichana wa Chibok aliyeokolewa Amina Ali
Nkeki, mtoto wake msichana wa miezi minne na mamake katika ikulu ya rais
mjini Abuja.
Rais Buhari amesema kuwa ni furaha kubwa kuwa Amina
amepata uhuru wake na kuongeza kuwa serikali yake itafanya kila iwezalo
kuhakikisha kuwa ameishi maisha mazuri.Aidha amesema kuwa pia litakuwa jukumu la serikali kuhakikisha kuwa ameendelea na masomo yake.
Yeye ni miongoni mwa wasichana zaidi ya mia mbili wa shule ambao walitekwa kutoka shule yao mjini Chibok na ndiye wa kwanza kuokolewa.