Wafungwa watatu wameuawa wakati wa maandamano kwenye gereza moja lililo kusini mwa Thailand.
Karibu wafungwa 100 walishiriki katika ghasia hizo kwenye gereza moja lililo mkoa wa Pattani, ambazo zilidumu kwa muda wa saa sita.
Wafungwa hao kwanza walichoma majengo mawili ndani ya gereza hilo.
Wafungwa hao walikuwa wametangaza matakwa kadha ikiwemo kutembelewa zaidi na familia zao na pia kupewa fursa ya kutizama habari kwenye runinga.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni