Nyota wa mchezo wa
tenisi kwa upande wa wanawake Serena Williams alijitia ugonjwa baada ya
kula chakula cha mbwa saa chache kabla ya kufuzu katika robo fainali ya
mashindano ya Italian Open.
Serena alijaribu kula kijiko kimoja
cha chakula cha mbwa wake kabla ya kumshinda Mmarekani mwenzake
Christina McHale katika seti za moja kwa moja.
''Nilisema kwani kuna nini,nitajaribu kipande kimoja,kinaonja utamu'',alisema. ''Lakini mda mchache nililazimika kukimbia chooni kama ambaye ningezimia''.
''Chakula kilikuwa na ladha mbaya''.
''Kinaonja
kama dawa ya kusafisha nyumba''.Katika video ya Snap chat ,wiliams
alielezea kuwa alichukua samaki na wali uliokuwa katika chakula
kilichopewa mbwa katika hoteli aliyokuwa akilala. ''Nilijilazimisha kula'',alisema mchezaji huyo wa Marekani mwenye umri wa miaka 34.
''Sijui wanatia nini katika chakula hiki cha mbwa,lakini mbwa alikipenda sana
#Habari:Wananchi wa kijiji cha Mkomilo kata ya Okaoni wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro wametishia kuchoma moto nyumba za Polisi na kufunga kituo cha polisi Okaoni kwa madai kuwa askari waliopo katika kituo hicho wameshindwa kukabiliana na matukio ya uhalifu na hivyo kusababisha mwenyekiti wa kijiji hicho kuuawa karibu na kituo hicho bila kupata msaada wa polisi licha ya kupewa taarifa.
#source Radio one stereo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemuagiza Kamishna wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Ernesti Mangu kumpandisha cheo askari wa Usalama barabarani ambaye alitukanwa na Mke wa Waziri wakati akitekeleza majukumu yake ya kikazi.
Rais ameyasema hayo wakati akifungua Kikao cha Makamanda wa Polisi wa Mikoa. Aidha Rais Dr. Magufuli amesema ameshamuonya Waziri huo ambaye mke wake amemtukana askari wa Usalama Barabarani.
Wakati akitoa agizo hilo, rais amesema hakuna kiongozi au familia ya kiongozi iliyoko juu ya sheria.
Chanzo: TBC1
WATU wawili wanaosadikika kuwa ni majambazi ambao wametokea Njombe wameuwawa katika majibizano ya risasi na polisi baada ya kuvamia Pub ya Mama Siyovelwa iliyopo eneo la mtaa wa Ikulu mjini Iringa
Tukio hilo limetokea majira ya saa 10:45 jioni ya jana tarehe 30/04/2016 baada ya watu hao kuvamia Pub hiyo kwa lengo la kupora kabla ya raia wema kutoa taarifa polisi
Baadhi ya mashuhuda waliokuwepo eneo hilo wamesema kuwa watu hao walihofiwa mapema wakati wa kuingia eneo hilo ambapo inadaiwa walikuwa watatu na mmoja alijichanganya na Raia na kujificha.
Kazi kubwa iliyofanywa na polisi imefanikisha watu hao wawili waliokuwa na silaha kuuwawa bila raia wengine kujeruhiwa
Miili miwili ya watu hao wanaosadikika ni majambazi ambao baada ya kupekuliwa wamekutwa na tiketi za basi la Hapy National kutoka Njombe imepelekwa hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa
Taarifa zaidi utazidi kuzipata japo Njombe kuna mauwaji ya kutumia silaha ambayo yalitokea juzi