BREAKING NEWS

Jumamosi, 16 Julai 2016

Nyimbo kumi bora zaidi kwa harusi duniani


EdImage copyrightGETTY
Image captionEd Sheeran, 25, akiwa na mashabiki
Wimbo wa mapenzi wa mwanamuziki wa Uingereza Ed Sheeran unaongoza kwa kupendwa sana na watu kama wimbo wa kufungua jukwaa wakati wa harusi.
Kwa mujibu wa mtandao wa Spotify, ambao wamechunguza maelfu ya orodha ya nyimbo zinazosambazwa zaidi katika mtandao huo, wimbo wa Thinking Out Loud unaongoza.
Wimbo wa At Last wake Etta James ni wa pili nao wimbo wa Ray LaMontagne, You Are the Best Thing ni wa tatu.
Nyimbo nyingine maarufu zilizo kwenye orodha ya 50 bora duniani ni wimbo wake Frank Sinatra uitwao The Way You Look Tonight na wimbo wa Marry You wake Bruno Mars.
SheeranImage copyrightGETTY
Image captionJina halisi la Sheeran ni Edward Christopher "Ed" Sheeran
Nyimbo kumi zinazopendwa zaidi duniani kwa mujibu wa Spotify, mtandao unaowawezesha watu kusikiliza nyimbo moja kwa moja mtandaoni, ni:
  1. Thinking Out Loud - Ed Sheeran
  2. At Last - Etta James
  3. You Are the Best Thing - Ray LaMontagne
  4. All of Me - John Legend
  5. A Thousand Years - Christina Perri
  6. Make You Feel My Love - Adele
  7. I Won’t Give Up - Jason Mraz
  8. Everything - Michael Bublé
  9. Better Together - Jack Johnson
  10. Amazed - Lonesta

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

SOMA ZAIDI HAPA