Maafisa wa serikali ya Sudan Kusini wameiambia BBC kwamba wanamtambua waziri wa madini Taban Deng Gai kuwa makamu wa kwanza wa rais akichukua mahala pake Riek Machar ambaye alitoroka mji mkuu wa Juba baada ya mapigano makali mapema mwezi huu.
Hatahivyo msemaji wa Machar amesema kuwa wameukataa uteuzi wa Bwana Deng.
Bwana Deng alikuwa mpatanishi mkuu wa Machar na hatua yake ya kuchukua wadhfa huo unaonyesha kuwa wametofautiana, hivyobasi kuweka mgawanyiko katika upinzani ambao unazidi kutatiza juhudi za kupata amani nchini Sudan Kusini ,kulingana na wachanganuzi.
Takriban watu 300 walifariki katika mapigano mapema mwezi huu katika mji mkuu wa Juba,kati ya vikosi vilivyo vitiifu kwa Machar na mpinzani wake rais Salva Kiiir
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni