BREAKING NEWS

Jumamosi, 16 Julai 2016

Bikizee wa miaka 94 arejea kazini Marekani


SoskinImage copyrightAP
Image captionBi Soskin (kati) alipokelewa kwa furaha kuu na wafanyakazi wenzake
Mama mmoja Mmarekani mwenye umri wa miaka 94 amerudi kazini kama askari waitwao Park Pangers wa kuhuduma katika mbuga na hifadhi za kitaifa nchini Marekani.
Bi Betty Reid Soskin, alikuwa ameacha kazi baada ya mkasa kumkumba ulimfanya.
Katika mkasa huo mwizi alimvamia nyumbani kwake tarehe 27 Juni, akamgonga ngumi kichwani na kumwibia simu, tarakilishi, vito vya thamani na hata medali yake aliyokuwa ametunukiwa na rais Obama.
Lakini anasema alitaka sana kurejelea maisha aliyoyazoea.
Bi Soskin, alikuwa mwelekezi katika hifadhi ya kihistoria iliyoko eneo la San Francisco Bay kwa muda wa miaka 10.
Kama anavyoonekana katika picha hizo za makaribisho ya wafanyikazi wenzake hapo hifadhi ya Rosie the Riveter World War Two Home Front National Historical Park ni vigumu kukadiria umri wakeread more.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

SOMA ZAIDI HAPA