.
Na; Martin Maranja Masese.
Vijana ndiyo nguvu kazi ya Taifa lolote lenye maendeleo katika Dunia hii.. lakini asilimia kubwa ya vijana hivi sasa wameathirika na utumiaji wa dawa za kulevya kutokana na hali hii Taifa linabaki halina maendeleo zaidi ya kurudi nyuma.
Tatizo la madawa ya kulevya limetokea kuwa janga kubwa duniani kote, watu wengi
wameathirika na janga hili.
Jinsia zote wanaume, wanawake, na vilevile makundi rika yote vijana na wazee pia.
Tatizo la dawa za kulevya linahusisha uendelezaji matumizi sugu ya dawa hadi kufikia tabia ya kutafuta
dawa za kulevya, kuwa katika hatari ya kurejelea matumizi na upungufu wa uwezo wa kukabiliana na visisimuaji vya kuridhisha kwa kawaida.
Utegemezi wa dawa za kulevya ni hali ya kuugua au isiyo ya kawaida ambayo hutokana na matumizi ya dawa ya mara kwa mara.
Taasisi inayoshughulika na Mwongozo wa Utambuzi na Takwimu ya Matatizo ya Akili imebainisha hatua tatu za utegemezi wa dawa za kulevya:
》kujihusisha/kutarajia, 》unywaji/ulevi,
》kuacha athari mbaya .
Hapa nitaeleza aina mbili za madawa ya kulevya yaani 'Cocaine' na 'Heroin'.
Cocaine hutokana na majani ya mmea uitwao kitaalamu Erythroxylum coca bush. Aina hii ya dawa ya kulevya hutolewa kwa mifumo ifuatayo;
》Unga ambapo mitaani hujulikana kama 'coke' na hutumika kwa kuvutwa puani kama unga, au kuyeyushwa na maji na kuchomwa kwenye mshipa wa damu.
》Crack ambapo mitaani hujulikana kwa jina hilohilo crack au rock, na hutengenezwa
kwa kuchanganywa na kemikali. Na hutumika kwa kuvutwa kama sigara.
Mara tu baada kutumia dawa hii dalili zifuatazo hutokea..,
>Mishipa ya damu husinyaa (constricted blood vessels)
>Joto la mwili huongezeka
>Mapigo ya moyo huongezeka
>Shinikizo la damu
>Dilated pupils
Heroin hujulikana vilevile kama 'diamorphine', hutokana na
mmea huitwao kitaalamu opium poppy.
Heroin kwa mfumo wa Morphine hutumiwa hospitalini kama dawa ya maumivu makali ya ghafla (acute pain) kwenye maumivu makali ya kifua wakati wa shambulizi la moyo, na kwa maumivu ya mtu aliyepata ajali, vilevile baada ya upasuaji, na maumivu sugu kwenye kansa. Hivyo hutolewa kwa kuangalifu mkubwa.
Dalili ambazo hutokea mara tu anapotumia Heroin:
> Kujisikia mwenye furaha na raha.
> Kupishana Kusikia hali usingizi na tahadhari.
> Midomo kuwa mikavu.
>Misuli kuishiwa nguvu.
>Kuhema polepole.
>Warm skin flushing.
>Mikono na miguu kuwa mizito.
>kope za macho kulegea.
Aina hii ya dawa ya kulevya huweza kutumika kwa kuvuta kwa pua, kuvuta kama sigara na kwa kuchoma kwenye mshipa.
Siku hizi watu hutumia njia ya haja kubwa na kwenye uke, ambapo kuta hufyonza heroin na kuanza kufanya kazi ndani ya sekunde arobaini.
Vijana walio wengi, wanajiingiza katika utumiaji wa dawa za kulevya kutokana na;
(i) umasikini katika familia zao. Haswa pale ambapo familia inakuwa haina dira. Ansjitolea mmoja kuikomboa.
(ii) kufiwa na wazazi wote wawili na kukosa mtu wa kumuongoza katika maisha yake.
(iii) vishawishi kutoka kwa marafiki kijana anajikuta ameacha shule na kujiingiza katika utumiaji wa dawa za kulevya.
(iv) Msongo wa mawazo haswaa baada ya kumaliza masomo yake na kisha hakuna ajira rasmi anayoipata.. anaanza kutumia dawa za kulevya.
(v) ulimbukeni.. hii ni tabia ya binadamu kupenda kuiga kila kitu ambacho nafsi na macho yake hutamani.
Madhara ya matumizi ya muda mrefu wa dawa za kulevya ni kama;
> Maambukizi ya magonjwa ya zinaa. Hii hutokana zaidi na matumizi ya sindano na vifaa vingine visivyo salama.
> Maambukizi kwenye kuta na milango ya moyo.
> Maambukizi ya ini na virusi (kama hepatitis C na HIV),
>Maambukizi ya figo.
>Maambukizi ya mfumo wa hewa.
>Maambukizi ya ngozi na majipu katika mwili.
Kuna aina nyingi za utumiaji wa dawa za kulevya..
vijana wengine wanavuta na wengine wanajichoma na sindano sehemu mbalimbali za mwili..
katika kutumia hiyo njia ya kujichoma hizo sindano wanaweza kutumia sindano moja zaidi ya watu wawili na kusababisha kuenea kwa ugonjwa wa UKIMWI endapo tu mtumiaji mmoja atakuwa ameathirika.
Vijana wengi wanaotumia dawa za kulevya hujikuta wakiishi katika mazingira ya taabu ikizingatiwa sehemu kubwa ya akili zao imetawaliwa na dawa hizo na wanapokosa kutumia hujiona kuna kitu wamepungukiwa (wataalam wanaita arosto) katika miili yao na wanapovuta hujiona wako ulaya na maisha wameyapatia.
Kulingana na ufafanuzi wa Shirika la Marekani la Tiba za
Ulevi, utegemezi wa dawa za kulevya hutofautiana na utegemeaji wa dawa na uzoefu wa dawa za kulevya.
Vilevile dawa hizi zinawatuma kufanya mambo ya ajabu mfano kuwaibia watu ,kubaka, matendo haramu n.k
Hata hivyo jamii inatakiwa kuwapatia msaada vijana hao bila kuwanyanyapaa kwani itapunguza madhara makubwa yanayosababishwa na waathirika hao..
Uwezekano wa kuacha kutumia dawa hizo ni mkubwa endapo watasaidiwa kuliko kutelekezwa..
Vijana wengi wanatamani kuachana na vitendo hivyo ila wanajikuta wapo katika mazingira magumu kwa kuwa hawajui sehemu ya kuanzia..
Kwa sababu, ili uanze kupata tiba.. ni muhimu kukubali kwamba madawa hayo yana athari kwako wewe mtumiaji..
Kisha baada ya hapo, hatua inayofuata ni kuanza kupata tiba ya kuachana na matumizi hayo ya dawa za kulevya.. ila kuna changamoto nyingi kwenye eneo hili..
(i) Dawa hazipatikani kwa urahisi.. dawa hizi ziko kwenye vituo maalum vya kutolea tiba hizo.. hivyo hazijazagaa mitaani.
(ii) vituo havipatikani kwa wepesi.., vituo vya tiba ya kuachana na dawa za kulevya.. havipo kwa wingi katika maeneo mengi.. hivyo, watumiaji huangaika katika kutafuta huduma.. haswa nje ya mkoa wa Dar es salaam.
(iii) Gharama za kupata huduma ni kubwa sana,,nimewahi kuwasikia wadau mbalimbali wakiomba ruzuku katika dawa hizi.. yaani ziingizwe nchini bila malipo au kwa gharama ndogo ili zitibu wengi..
Hivyo kuna haja ya serikali kulitizama suala hilo kwa lengo la kutatua tatizo hilo...
Hatuwezi kuendelea kukaa kimya. Taifa letu linaaibika vibaya sana... Inaudhi, inakera na inatuongezea chuki sana kwa serikali iliyo madarakani. hii ni aibu kubwa kwa Taifa.
Nimeangalia hivi sasa serikali yetu imesahau jukumu la kulinda maisha ya watanzania
hasa tatizo la madawa ya kulevya.
Tatizo limekuwa kubwa kiasi kwamba siku hizi huhitaji nguvu
kuyapata.
Vijana wale wanaotumia, ukizungumza nao wanasema unaweza kupiga simu ukaagiza mzigo na ukaletewa.
Kitengo cha kupambana na dawa za kulevya mmelala?
Je, mmekubali kuwa Tanzania iendelee kuwa 'conduit' yaani bomba la kusafirishia dawa za kulevya kwenda ughaibuni??
Raisi wetu (aliyemaliza muda wake) wa Jamhuri ya muungano, aliwahi kukaririwa akisema, anayo majina ya wauza madawa ya kulevya nchini.., sijui yalikwenda wapi majina hayo..
Watu wanaokamatwa viwanja vya ndege na dawa za kulevya ni vidagaa vya madawa ya kulevya, Nyangumi na mapapa wametulia tu wanatuaharibia vijana wetu.
Vijana wengi wanakubali kutumika kufanya biashara hii kwa sababu ya ugumu wa maisha..wanaingia kwenye biashara hii kwa kutaka mafanikio ya haraka kwenye maisha yao..
Madawa ya kulevya ni tatizo sugu sana nchini, ila inavyoonekana, hakuna ambaye anajali tena hilo.. watu wameamua kukubali athari zake na wanaishi tu... Taifa linapoteza nguvu kazi.. Taifa limeshindwa kuwaokoa vijana..
Madawa ya kulevya yanaingizwa nchini kiulaini kama dhahabu inavyopelekwa nje ya nchi... Tanzania imekuwa ni soko la madawa ya kulevya.. watuhumiwa wapo.. ila hata hawashughulikiwi..
Madawa ya kulevya yanaathiri sana vijana. Kutokana na hali
ngumu ya maisha, na pia kutokana na biashara hiyo
kuendeshwa na watu ambao wana "status" kubwa sana kwenye jamii,.. vijana wanashawishika kirahisi
sana kujiingiza kwenye hiyo biashara.
Inawezekana kabisa kuwa vinara wa hiyo biashara wanajulikana na vyombo husika lakini hawachukuliwi hatua zozote either kwa sababu ni "watu wakubwa sana" in whatever sense or wanaotakiwa kuwachukulia hatua ni sehemu ya hiyo biashara.
Nasema hivyo kwa sababu siyo kawaida kwa hao wanaokamatwa na dawa hizo kuweza kumiliki takribani kilo 150 za madawa ya kulevya.
Wengi naamini walikuwa ni
wasafirishaji tuu... mfano yule Agness Masogange, Jackline Pentaziel na wengineo..
Mbaya zaidi wamiliki wa hii biashara wanawatumia sana vijana na wakikamatwa wanaachwa kwenye mataa., vijana wenyewe hawawezi kutaja 'mabosi' wao, wakiogopa maisha yao na familia zao kuwa rehani..
Mwaka 2010 kuna mabondia wa Kitanzania waliwahi kufungwa huko nchini Mauritius, kifungo cha miaka 15 baada ya kupatikana na kosa la kuingiza madawa ya kulevya nchini humo:,
soma hiyo habari hapa.. http://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-sheria-the-law-forum/473554-watanzania-wanne-wafungwa-miaka-15-mauritius.html .
Hawa mabondia walikwenda kama wanamichezo lakini kumbe walikuwa na agenda
nyingine kubwa zaidi ya siri..
Kuna yule mwanamuzi aliyefariki huko Afrika Kusini ambaye naye inasemekana sababu ni madawa ya kulevya..., inasemekana alitumia dawa za kulevya kuliko ilivyo kawaida..
Kuna Mtanzania mwingine mwanamke, alikutwa amefariki kwenye hoteli aliyofikia huko nchini Italia, ilikuwa ni Mwezi Juni, 2013., baada ya madawa aliyokuwa amebeba kupasukia tumboni.
Kuna Mtanzania alikamatwa na madawa ya kulevya nchini Marekani mwaka jana.
Mwezi Februari, 2013 kulikuwa na habari za mwanamuziki wa
Bongo Fleva kukamatwa na madawa ya kulevya nchini Burundi:
Soma hiyo habari hapa http://www.jamiiforums.com/celebrities-forum/407776-timbulo-akamatwa-na-madawa-ya-kulevya-burundi-cheki-picha-za-tukio-hapa.html
Tumewahi pia kusikia kuhusu Mtanzania aliyekamatwa na
madawa ya kulevya huko nchini Misri japokuwa yeye baadae alikana kuwa siyo Mtanzania.
Mwaka 2013 tulipata taarifa kuwa kuna wanawake wawili raia wa Tanzania wametambuliwa kuwa ndiyo wanaodaiwa kuingiza shehena ya dawa za kulevya zenye thamani ya zaidi ya Sh. bilioni 6.8 nchini Afrika Kusini wakitokea Tanzania.
Pia Kuna mtanzania mwingine aliyewahi kufungwa miaka 8 huko nchini Angola baada ya kupatikana na madawa ya kulevya aliyokuwa akisafirisha kwenda Afrika Kusini.
Inadaiwa huyu Mtanzania aliondoka Afrika Kusini na kwenda kufuata dawa za kulevya Brazil na akafanikiwa kuchukuwa ila wakati anarudi Afrika Kusini kwenye kubadilisha ndege Angola alikamatwa na kukutwa na dawa za kulevya miaka mitatu iliyopita.
Sasa hivi.. watanzania hawaogopi kubaguliwa kwa sababu ya rangi yao kwenye nchi za wenzetu.. ila wanaogopa kwa aibu ambayo wanaipata wanapoonekana kama wasafirishaji wa dawa za kulevya kila waendako..
Kwa takwimu zilizopo nchini China.. watanzania wanaongoza kufungwa kwa wingi nchini humo kwa tuhuma za kusafirisha na kuingiza dawa za kulevya.. katika nchi za Afrika mashariki na kati, zinafuata Kenya, Uganda na pia Sudan.. hii ni hatari sana..
Naweza kuandika zaidi ya kurasa 45 kuhusu mambo haya.. serikali ina dhamana kubwa sana kwenye jambo hili.. inapaswa kufanya yafuatayo ili kutokomeza biashara haramu ya dawa za kulevya nchini..
》kuanzisha kampeni kubwa kwenda kwa wananchi kuhusu athari za wazi za dawa hizi.
》kitengo cha kuzuia na kupambana na dawa za kulevya.. kihakikishe kinafanya kazi ya watanzania nasiyo wafanyabiashara wa shughuli hiyo..
》Adhabu kali zitoke kwa wale wanaokamatwa na wanaojihusisha na shughuli hii.
》Kwa sababu maskani na magenge yanajulikana.. yaharibiwe na kukamata wahusika..
》Muswada wa kunyonga wale wote wanaokamatwa na dawa hizi au wafanyabiashara wa shughuli hizi.. wanyongwe au wapigwe risasi hadi kufa.
》Serikali sasa iache tabia ya kukamata na kuwafunga watumiaji ila ikamate wale wafanyabiashara wenyewe.
》Ukaguzi kwenye bandari na mipaka yetu.. unapaswa kuimarishwa ili kutoruhusu uingizwaji wa dawa hizi kutoka nje ya nchi.
#SayNoToDrugs
#SayNoToDrugs
#SayNoToDrugs
#SayNoToDrugs
#SayNoToDrugs
#SayNoToDrugs
(Imeandikwa kwa msaada wa mabandiko na machapisho mbalimbalo ya ndani na nje ya nchi)
Martin Maranja Masese,
Mwananchi wa kawaida,
martinchizzle@gmail.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni