BREAKING NEWS

Alhamisi, 12 Mei 2016

Rais wa Brazil Dilma Rousseff asimamishwa kazi

 
Bunge la Seneti Brazil limepiga kura kuamua kuidhinisha kura ya kutokuwa na imani dhidi ya kiongozi wa taifa hilo Dilma Rousseff.
Atasimamishwa kazi ya urais kwa siku zisizozidi 180 wakati bunge hilo la Seneti litakagua tuhuma zinazomkabili.
Bi Rousseff anatuhumiwa kubadili kinyume cha sheria fedha za serikali kuficha nakisi inayoongezeka ya umma kufuatia kuchaguliwa kwake tena mnamo 2014, tuhuma anazozikana.
Masenata 55 waliunga kuidhinishwa kura hiyo ya kutokuwana imani dhidi ya 22 bungeni katika kikao cha zaidi ya saa 20.
Makamu wa rais Michel Temer sasa ndio atashikilia madaraka wakati kesi dhidi ya Bi Rousseff inaendelea.
Rousseff alichukua hatua ya mwisho kujiokoa kwa kukataa rufaa katika mahakama ya juu zaidi nchini humo kusitisha kura hiyo, lakini hatua hiyo ilipingwa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

SOMA ZAIDI HAPA