WATU wawili wanaosadikika kuwa ni majambazi ambao wametokea Njombe wameuwawa katika majibizano ya risasi na polisi baada ya kuvamia Pub ya Mama Siyovelwa iliyopo eneo la mtaa wa Ikulu mjini Iringa
Tukio hilo limetokea majira ya saa 10:45 jioni ya jana tarehe 30/04/2016 baada ya watu hao kuvamia Pub hiyo kwa lengo la kupora kabla ya raia wema kutoa taarifa polisi
Baadhi ya mashuhuda waliokuwepo eneo hilo wamesema kuwa watu hao walihofiwa mapema wakati wa kuingia eneo hilo ambapo inadaiwa walikuwa watatu na mmoja alijichanganya na Raia na kujificha.
Kazi kubwa iliyofanywa na polisi imefanikisha watu hao wawili waliokuwa na silaha kuuwawa bila raia wengine kujeruhiwa
Miili miwili ya watu hao wanaosadikika ni majambazi ambao baada ya kupekuliwa wamekutwa na tiketi za basi la Hapy National kutoka Njombe imepelekwa hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa
Taarifa zaidi utazidi kuzipata japo Njombe kuna mauwaji ya kutumia silaha ambayo yalitokea juzi
Jumamosi, 30 Aprili 2016
MAJAMBAZI WAWILI WAUAWA IRINGA
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
SOMA ZAIDI HAPA
-
Magufuli apunguza kodi ya mapato na 2% Huku wafanyikazi kote duniani wakiadhimisha sikukuu ya wafanyakazi, nchini Tanzania, wafanyikazi wa...
-
Mwanamke ambaye anataka kutumia mayai ya uzazi ya bintinye ili kumzaa mjukuu wake ameshinda kesi mahakanani na kuruhusiwa kufanya...
-
Image caption Mosul Iraq Viongozi wawili wakuu wa kundi la kigaidi la Islamic State waliuawa katika mashambulizi ya angani...
-
Mwanamume mmoja katika mji wa Bungoma, Magharibi mwa Kenya ameshangaza wengi baada...
-
👇👇👇👇👇👇 WALIMU wa shule ya msingi Kianda wameanza mgomo wa siku mbili wa kutofundisha shuleni hapo huku wakilaani kitendo cha Ofisa E...
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni