Nyota wa mchezo wa
tenisi kwa upande wa wanawake Serena Williams alijitia ugonjwa baada ya
kula chakula cha mbwa saa chache kabla ya kufuzu katika robo fainali ya
mashindano ya Italian Open.
Serena alijaribu kula kijiko kimoja
cha chakula cha mbwa wake kabla ya kumshinda Mmarekani mwenzake
Christina McHale katika seti za moja kwa moja.''Nilisema kwani kuna nini,nitajaribu kipande kimoja,kinaonja utamu'',alisema.
''Lakini mda mchache nililazimika kukimbia chooni kama ambaye ningezimia''.
''Chakula kilikuwa na ladha mbaya''.
''Kinaonja kama dawa ya kusafisha nyumba''.Katika video ya Snap chat ,wiliams alielezea kuwa alichukua samaki na wali uliokuwa katika chakula kilichopewa mbwa katika hoteli aliyokuwa akilala.
''Nilijilazimisha kula'',alisema mchezaji huyo wa Marekani mwenye umri wa miaka 34.
''Sijui wanatia nini katika chakula hiki cha mbwa,lakini mbwa alikipenda sana
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni