Wapinzani wa klabu ya Young Africans, katika michuano ya kuwania Kombe la Shirikisho Barani Afrika, Medeama kutoka Ghana, wametua Dar es Salaam tayari kwa mechi baina ya timu hizo Jumamosi.
Wachezaji hao waliwasili Dar Alhamisi na wakafanya mazoezi katika uwanja wa Karume.
Yanga itaikaribisha Medeama kwa mchezo wa tatu kuwania taji hilo hatua ya makundi katika uwanja wa taifa Dar es Salaam.
Mchezao huo utaanza saa 10.00 jioni
Michezo miwili ya awali ya Yanga katika michuano hiyo ilikuwa ni dhidi ya Mo Bejaia ya Algeria ambako ilipoteza kwa bao 1-0 kabla ya kupoteza tena dhidi ya TP Mazembe, mechi iliyopigwa jijini Dar es Salaam.
Mchezo wa Jumamosi utachezeshwa na waamuzi kutoka Misri ambao ni Ibrahim Nour El Din atakayekuwa mwamuzi wa kati; akisaidiwa na Ayman Degaish na Samir Gamal Saad wakati mwamuzi wa akiba akiwa ni Mohamed Maarouf Eid Mansour, kwa mujibu wa Shirikisho la Kandanda la Tanzania (TFF)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni