BREAKING NEWS

Jumatatu, 11 Julai 2016

Mwanamke apinga udhalimu wa polisi Marekani


Image copyrightJONATHAN BACHMANREUTERS
Image captionMwanamke apinga udhalimu wa polisi Marekani
Maandamano nchini Marekani kupinga mauaji ya wanaume weusi na polisi wazungu yameendelea katika mji wa Baton Rouge, Louisiana.
Image copyrightAFP
Image captionMakumi ya waandamanaji walikamatwa na polisi
Makumi ya waandamanaji walikamatwa huku polisi wakiendeleza sera yao ya kuwakamata kamata weusi wanaopinga mauaji hayo ya polisi.
Image copyrightAP
Image captionViongozi wa vuguvugu la Black Lives matter walikamatwa
Matukio ya makabiliano hayo yameibua hofu ya kuenea kwa uhasama na ubaguzi wa rangi.
Hata hivyo picha moja imeibua hisia kali kwenye mitandao ya kijamii kote duniani.
Image copyrightREUTERS
Image captionPolisi wameendeleza kauli ya kuwa na msimamo mkali dhidi ya weusi
Picha hiyo inaonesha maafisa wawili wa polisi waliojihami hadi kwenye kisigino wakijiandaa kumkabili kipusa mmoja mweusi ambaye hakuwa amejihami kwa namna yeyote ila kwa ujasiri wa kupinga mauaji hayo ya wanaume weusi jumanne iliyopita.
Image captionPicha hiyo ya mwanamke huyo imefananishwa na ile ya ''Tank Man'' ya China
Picha hiyo ilipigwa na mpiga picha wa shirika la habari la Reuters Jonathan Bachman, ambaye ni mkaazi wa mji wa New Orleans.
Image copyrightREUTERS
Image captionmakumi ya waandamanaji walikamatwa
Waamerika wengi waliosambaza picha hiyo wameifananisha na ile picha ya mwanaume aliyekuwa akipigania haki za wenyeji nchini China wakati walipokabiliwa na wanajeshi wakiwa wamejihami na vifaru vya kijeshi.
Wapiganiaji haki za kibinadamu na haswa haki za wamarekani weusi wamekuwa wakijadili sadfa ya kuwa taifa linalodai kuwa kitovu cha demokrasia kinatumia mbinu za kidhalimu zilizotumika mataifa ya kikomunisti karne iliyopita.
Image copyrightREUTERS
Image captionwanaume weusi wamejipata pabaya mikononi mwa polisi wazungu
Mpiganiaji haki za weusi Shaun King ambaye pia ni mwandishi wa jarida la New York Daily anasema kuwa ni jambo la kufedhehesha mno mno kuwa picha hiyo ya kihistoria inatokea Marekani mwaka huu wa 2016, weusi wakipigana dhidi ya ubaguzi wa rangi.
Image copyrightAFP
Image captionAlton Sterling ambaye mauaji yake yaliibua maandamano Marekani
Kipusa huyo anadaiwa kukamatwa na polisi lakini hakuna anayemfahamu wala anayejua kilichomkuta mikononi mwa polisi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

SOMA ZAIDI HAPA