BREAKING NEWS

Ijumaa, 8 Julai 2016

Marekani na Korea Kusini wajilinda dhidi ya Korea Kaskazini


Mfumo wa THAADImage copyrightAFP
Image captionMfumo wa kujilinda na mashambulio ya makombora(THAAD)
Marekani na Korea Kusini zimekubaliana kuweka mfumo wenye utata wa ulinzi dhidi ya makombora, kama njia ya kukakabiliana na vitisho vinayoendelea kutoka kwa Korea kaskazini.
Mfumo huo wa ulinzi unaowekwa katika maeneo yenye milima mirefu kudhibiti mashambulizi ya makombora utawekwa kujibu vitisho tisho kutoka Pyongyang, ilieleza taarifa.
Haijabainika wazi ni wapi mtambo huo utawekwa na hatimae ni nani ataudhibiti.
Image copyright
Image captionNamna mfumo wa kukabiliana na Makombora (THAAD) unavyofanya kazi
Uchina, ambayo imekuwa ikipinga mara kwa mara mpango huo, imepinga mfumo huo tena kupitia wajumbe wa korea Kusini na Marekani.
Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Uchina amesema kuwa mfumo wa THAAD utadhuru amani na utulivu katika kanda hiyo, licha ya uwezo wake wa kugundua na kulipua makombora ya Korea Kaskazini.
"Uchina inaelezea kutoridhishwa kwake na kupinga vikali hili'', ilisema katika taarifa kupitia mtandao wake.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

SOMA ZAIDI HAPA