Virusi vya hepatitis vinaua watu wengi zaidi ya Ukimwi na hata maradhi ya kifua kikuu, utafiti wa miaka 23 umebaini.
Kwa mujibu wa utafiti huo uliochapishwa katika jarida la Lancet, maambukizi ya virusi vya hepatitis vilisababishavifo vya watu milioni moja u nusu mwaka wa 2013 licha ya kuweko kwa madawa na hata chanjo dhidi yake.
''Mwaka wa wa 2013 watu 1.45 walipoteza maisha yao kutokana na Hepatitis.''
kwa mujibu wa takwimu iliyokusanywa na shirika la afya duniani WHO mwaka huo kulikuwa na vifo vya watu milioni moja nukta mbili (1.2) kutokana na maradhi yanayosababishwa na Ukimwi.
Aidha WHO inasema kuwa wakati huohuo yaani mwaka wa 2014 kulikuwa na takriban vifo 1.5 milioni kutokana na ugonjwa wa kifua kikuu.
Kutokana na utafiti huuu sasa WHO imeanza kupanga mikakati ya kupigana na virusi hivyo vya Hepatitis.
Watafiti wanasema kuwa kuna haja ya dharura sasa kwa mipango hiyo ya WHO ya kukabiliana na virusi hivyo vya Hepatitis.
Virusi vya Hepatitis ni vingi na huambukizwa kwa njia nyingi na hivyo kugawanywa katika vitengo vitano yaani A, B, C, D, E.
Virusi vya Hepatitis A na E vinaambukizwa kupitia ka maji na vyakula vilivyoambukizwa.
Virusi vya Hepatitis B na C ndivyo vinavyosababisha idadi kubwa zaidi ya vifo kutokana na kuwa vinasababisha kudhohofika kwa maini na hata kusababisha mgonjwa kuambukizwa saratani ya ini.
Wanasayansi walifanya utafiti huo katika mataifa 183 kuanzia mwaka wa 1990 hadi mwaka wa 2013.
Watafiti hao kutoka vyuo vikuu vya Imperial College London na chuo kikuu cha Washington waligundua kuwa idadi ya vifo vinavyosababishwa na virusi vya Hepatitis vimeongezeka kwa asilimia 60% katika kipindi hicho.
''Ni ajabu kuwa maradhi haya ambayo tuna madawa yake ndiyo yanayouwa zaidi haswa katika maytaifa yenye utajiri mkubwa.'' alisema profesa mmoja wa chuo cha Imperial College London Dr Graham Cooke
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni