Kundi moja la
maafisa wa polisi limefanya maandamano karibu na tamasha lililofanyika
katika mji wa nyumbani wa nyota wa muziki Beyonce huko Houston.
Wanachama
wa muungano wa polisi na Sherrif walisimama mbali na uwanja wa soka na
kuelekeza mwangaza wa bluu katika ukumbi wa tamasha hilo.Walikuwa wanapinga kanda ya video ya Beyonce ambayo wanasema inawaponza polisi.
Mwanachama mmoja wa polisi amekiambia chombo cha habari KHOU11 kwamba hawakufurahia baada ya Beyonce kutumia picha za gari moja la polisi mjini New Orleans iliokuwa ikizama katikamafuriko.
''Tunaamini kwamba baadhi ya mambo yake ni kinyume na maafisa wa polisi'',alisema.
''Mtu yoyote anyedhani kwamba siwapendi polisi anakosa kwa sababu'', alisema.
''Ninawapenda na kuwaheshimu sana polisi pamoja na familia za maafisa hao ambao hujitolea ili kuhakikisha tuko salama''.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni