BREAKING NEWS

Jumapili, 3 Julai 2016

Magufuli: AirTanzania kupaa tena Septemba


Image captionMagufuli: AirTanzania kupaa tena kufikia mwisho wa mwezi Septemba mwaka huu
Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametangaza kuwa shirika la ndege la Tanzania litarejea angani ''kabla ya mwisho wa mwezi Septemba Mwaka huu 2016''.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari na kaimu mkurugenzi wa mawasiliano ya ikulu ya Tanzania bw Gerson Msigwa
''Dkt. Magufuli amesema serikali yake imechukua hatua madhubuti za kulifufua shirika la ndege la Taifa.
Tayari mipango imefanywa kuhakikisha ndege mbili aina Bombadier Q400 zinanunuliwa na zitatua hapa nchini kabla ya mwisho wa mwezi Septemba Mwaka huu 2016.'' taarifa hiyo inaeleza.
Tamko hilo ni ishara nzuri kwa sekta ya uchukuzi nchini Tanzania na vilevile kanda nzima ya Afrika Mashariki ambayo imekuwa ikikabiliwa na gharama za juu za usafiri kutoka kwa mashirika ya kigeni.
BIASHARA NA RWANDA
Wakati huohuo rais Magufuli aliueleza ujumbe wa wafanyabiashara kutoka Rwanda kuwa China imeonesha nia ya kushirikiana na Tanzania kujenga reli ya kisasa yaani “Standard Gauge” kwa nia ya kurahisisha uchukuzi wa mizigo kutoka bandari ya Dar es salaam kwa manufaa ya wafanyabiashara.
Image captionMarais Paul Kagame na mwenyeji wake John Magufuli
''Tanzania imeamua kuipatia Rwanda eneo la kujenga bandari kavu kwa ajili ya mizigo ya wafanyabiashara wake na pia Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) itafungua ofisi mjini Kigali nchini Rwanda ikiwa ni juhudi za kurahisisha na kuongeza biashara kati ya nchi hizi mbili.''
Juhudi hizo bw Magufuli anasema ni kuwahakikishia wafanyabiashara wa Rwanda kuwa bandari ya Dar es salaam ni salama kwao kupitisha mizigo na ameahidi kuwa Serikali ya Tanzania inaendelea kuchukua hatua za kuimarisha bandari hiyo na kurahisisha biashara kati ya nchi hizi mbili.
Kwa upande wake rais Paul Kagame wa Rwanda alitoa wito kwa ''Tanzania na Rwanda pamoja na nchi nyingine za Jumuiya ya Afrika Mashariki kushirikiana na sekta binafsi katika kutumia fursa nyingi za kibiashara zilizopo baina yake na kuwaletea manufaa wananchi''

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

SOMA ZAIDI HAPA