Raia mmoja wa 
Thailand anaendelea kuuuguza jeraha katika hospitali moja baada ya nyoka
 aina ya chatu kutokea ndani ya choo na kumng'ata uume wake.
Attaporn
 Boonmakchuay,ambaye alipoteza damu nyingi amesema kuwa nyoka hiyo 
ilikuwa ikimvuta baada ya yeye na mkewe kujaribu kuipiga.Madaktari wanasema kuwa Bw Attaporn ambaye alipoteza damu nyingi anaendelea vyema na matibabu.
Kisa hucho kilitokea wakati ambapo Attaporn mwenye umri wa miaka 38 alielekea katika choo chake nyumbani kwake huko Chachoengsao,mashariki mwa Bangkok kabla ya kwenda kazini siku ya Jumatano.
Wakati alipokuwa akitumia choo hicho alihisi uchungu mkali.
 
 
 
 
 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni