BREAKING NEWS

Jumatatu, 4 Julai 2016

Ugaidi: Facebook yatambua waliovamia Bangladesh


Image copyrightAP
Image captionWaziri mmoja amesema watu hao walikuwa kwenye kundi la Mujahdeen Bangladesh wala sio Islamic State.
Maafisa wa usalama nchini Bangladeshi wametumia mtandao wa kijamii wa Facebook kuwatambua watatu kati ya magaidi 6 walioshambulia mji mkuu wa Dhaka.
Polisi wanaochunguza shambulizi hilo baya zaidi la kigaidi kuwahi kutokea nchini humo wanasema Facebook imewasaidia sana.
Afisa hao wa polisi wametangaza hayo huku nchi hiyo ikianza siku mbili za maombolezo.
Image copyright
Image captionUgaidi: Facebook yatambua magaidi waliovamia Bangladesh
Ingawa kundi la wapiganaji la Islamic State limesema lilitekeleza shambulio hilo, ambalo lilimalizika baada ya makamando walipovamia jengo la mkahawa jana asubuhi.
Waziri mmoja amesema watu hao walikuwa kwenye kundi la Mujahdeen Bangladesh wala sio Islamic State.
Watu 20 waliuwawa, wengi wao wageni, pamoja na askari polisi wawili.
Image copyrightAP
Image captionWakuu wanasema washambuliaji wote walikuwa waBangladeshi, na walikuwa wakisakwa na maafisa wa usalama
Wakuu wanasema washambuliaji wote walikuwa waBangladeshi, na walikuwa wakisakwa na maafisa wa usalama
Wapiganaji sita waliuwawa na mmoja alikamatwa

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

SOMA ZAIDI HAPA