BREAKING NEWS
-
Shule 10 zilizofanya vizuri: 1.Kisimiri,-Arusha 2.Feza Boys,-Dar es Salaam 3.Alliance Girls,-Mwanza 4. Feza Girls,-Dar es Salaam 5. Ma...
-
Image copyright PA WIRE Image caption George Osborne Waziri wa fedha wa Uingereza George Osborne ameeleza mipango ya wizara yake ...
Alhamisi, 5 Januari 2017
Trump kuondoa sheria ya afya ya Obamacare Marekani
Jumatatu, 5 Septemba 2016
Majina mashuhuri zaidi ya watoto
TJina Noah limeingia kwenye orodha ya majina 10 mashuhuri zaidi kwa kupewa watoto wavulana kwa mara ya kwanza, huku Amelia likisalia kuwa jina ambalo wazazi wengi wanawapa watoto wasichana England na Wales, taasisi ya taifa ya Takwimu Uingereza imeonesha.
Jina Oliver ndio linaloongoza upande wa wavulana, likishikilia nafasi ya kwanza tangu 2013 nalo Amelia likiwa juu kwa wasichana tangu 2011. Watoto walioitwa Oliver mwaka 2015 ni 6,941 na Amelia 5,158.
Maafisa wa ONS waliorodhesha majina kando kwa mujibu wa jinsi jina liliandikwa.
Iwapo majina yanayotamwa kwa njia sawa yangewekwa pamoja, basi orodha hiyo huenda ingelikuwa tofauti kidogo.
Mfano ni jina Muhammad ambalo linashikilia nafasi ya 12 likiwa na watoto 3,730.
Kuna wazazi walioandika jina hilo kama Mohammed (2,332) na wengine kama Mohammad (976). Iwapo majina hayo yangejumlishwa, basi jina hilo lingelikuwa katika 10 bora.
Yalikuwepo majina ya kushangaza. Kwa mfano watoto wavulana 17 na wasichana 15 walipewa jina Baby.
Majuzi, utafiti ulionesha karibu sehemu moja kati ya tano ya wazazi Uingereza wanajutia majina waliyowapa watoto wao.
Wavulana 35 walipewa jina Rocky, na 21 wakapewa Apollo, labda kutokana na wahusika wakuu wa filamu ya ndondi Rocky Balboa na Apollo Creed.
Wavulana 15 walipewa jina Blue na wengine 14 wakaitwa Ocean. Na kunao 18 walipewa jina Blu.
Kuna jumla ya wavulana 36 ambao watahitajika kujifunza kuandika na kutamka jina lao, Tymoteusz.
Upande wa wasichana 280 walipewa jina Arya, mmoja wa wahusika wakuu filamu ya Game of Thrones, na wengine 562 wakaitwa Aria, 33 Ariah, 17 Aaria na sita Aariah, jina ambalo huenda ni moja ila likaandikwa tofauti.
Jina Kaleesi, pia kutoka kwa filamu hiyo, lilipewa wasichana watano.
Jina Princess lilipewa wasichana 72, ikikaribia wavulana 77 walioitwa Prince.
Takwimu hizo zinaonesha jina Oliver ndilo maarufu zaidi kwa wavulana maeneo yoteb ya Englandisipokuwa London na West Midlands, ambapo jina Muhammad linaongoza.
Jina Muhammad lilipita Oliver eneo la West Midlands mwaka 2014.
Majina mashuhuri zaidi 2015
- Oliver 6,941
- Jack 5,371
- Harry 5,308
- George 4,869
- Jacob 4,850
- Charlie 4,831
- Noah 4,148
- William 4,083
- Thomas 4,075
- Oscar 4,066
Majina maarufu kwa wasichana 2015
- Amelia 5,158
- Olivia 4,853
- Emily 3,893
- Isla 3,474
- Ava 3,414
- Ella 3,028
- Jessica 2,937
- Isabella 2,876
- Mia 2,842
- Poppy 2,816
Wasichana 72 walipewa jina Adele, 39 wakaitwa Paloma, kutokana na mwanamuziki Paloma Faith.
Kulikuwa na wasichana 35 walioitwa Rihanna, na tisa Rhianna.
Majina 50 mashuhuri zaidi ya wavulana na wasichana England na Wales mwaka 2015 | |||||
---|---|---|---|---|---|
Wavulana | Wasichana | ||||
Nambari | Jina | Watoto | Nambari | Jina | Watoto |
1 | OLIVER | 6941 | 1 | AMELIA | 5158 |
2 | JACK | 5371 | 2 | OLIVIA | 4853 |
3 | HARRY | 5308 | 3 | EMILY | 3893 |
4 | GEORGE | 4869 | 4 | ISLA | 3474 |
5 | JACOB | 4850 | 5 | AVA | 3414 |
6 | CHARLIE | 4831 | 6 | ELLA | 3028 |
7 | NOAH | 4148 | 7 | JESSICA | 2937 |
8 | WILLIAM | 4083 | 8 | ISABELLA | 2876 |
9 | THOMAS | 4075 | 9 | MIA | 2842 |
10 | OSCAR | 4066 | 10 | POPPY | 2816 |
11 | JAMES | 3912 | 11 | SOPHIE | 2779 |
12 | MUHAMMAD | 3730 | 12 | SOPHIA | 2744 |
13 | HENRY | 3581 | 13 | LILY | 2711 |
14 | ALFIE | 3540 | 14 | GRACE | 2658 |
15 | LEO | 3468 | 15 | EVIE | 2529 |
16 | JOSHUA | 3394 | 16 | SCARLETT | 2285 |
17 | FREDDIE | 3219 | 17 | RUBY | 2215 |
18 | ETHAN | 2940 | 18 | CHLOE | 2158 |
19 | ARCHIE | 2912 | 19 | ISABELLE | 2119 |
20 | ISAAC | 2829 | 20 | DAISY | 2113 |
21 | JOSEPH | 2786 | 21 | FREYA | 2090 |
22 | ALEXANDER | 2759 | 22 | PHOEBE | 2081 |
23 | SAMUEL | 2705 | 23 | FLORENCE | 2053 |
24 | DANIEL | 2622 | 24 | ALICE | 2006 |
25 | LOGAN | 2610 | 25 | CHARLOTTE | 1951 |
26 | EDWARD | 2593 | 26 | SIENNA | 1941 |
27 | LUCAS | 2448 | 27 | MATILDA | 1774 |
28 | MAX | 2407 | 28 | EVELYN | 1770 |
29 | MOHAMMED | 2332 | 29 | EVA | 1753 |
30 | BENJAMIN | 2328 | 30 | MILLIE | 1673 |
31 | MASON | 2263 | 31 | SOFIA | 1640 |
32 | HARRISON | 2241 | 32 | LUCY | 1525 |
33 | THEO | 2103 | 33 | ELSIE | 1513 |
34 | JAKE | 2013 | 34 | IMOGEN | 1478 |
35 | SEBASTIAN | 1988 | 35 | LAYLA | 1428 |
36 | FINLEY | 1978 | 36 | ROSIE | 1403 |
37 | ARTHUR | 1966 | 37 | MAYA | 1354 |
38 | ADAM | 1903 | 38 | ESME | 1340 |
38 | DYLAN | 1903 | 39 | ELIZABETH | 1338 |
40 | RILEY | 1728 | 40 | LOLA | 1322 |
41 | ZACHARY | 1644 | 41 | WILLOW | 1308 |
42 | TEDDY | 1430 | 42 | IVY | 1275 |
43 | DAVID | 1394 | 43 | ERIN | 1249 |
44 | TOBY | 1363 | 44 | HOLLY | 1248 |
45 | THEODORE | 1302 | 45 | EMILIA | 1243 |
46 | ELIJAH | 1294 | 46 | MOLLY | 1215 |
47 | MATTHEW | 1279 | 47 | ELLIE | 1185 |
48 | JENSON | 1223 | 48 | JASMINE | 1182 |
49 | JAYDEN | 1219 | 49 | ELIZA | 1171 |
50 | HARVEY | 1190 | 50 | LILLY | 1146 |
Kiir akubali wanajeshi wa UN watumwe Juba, Sudan Kusini
Bw Kiir alikuwa awali amekataa kutumwa kwa wanajeshi hao 4,000 kutoka mataifa ya kanda, akisema huo ni ukiukaji wa uhuru wa Sudan Kusini.
UN iliidhinisha kutumwa kwa wanajeshi hao baada ya kuzuka upya kwa vita baina ya wanajeshi waaminifu kwa Bw Kiir na aliyekuwa makamu wake wa rais Dkt Riek Machar mwezi Julai mjini Juba.
Kikosi hicho cha ziada kitakuwa na mamlaka zaidi kushinda kikosi cha sasa cha wanajeshi 13,000 ambacho kimekuwa kikihudumu nchini humo
Jumatano, 3 Agosti 2016
JINSI YA KUPATA MTOTO WA JINSIA UNAYOTAKA
Habari za wakati huu ndugu yangu mpendwa na mfuatiliaji mzuri wa Makala zangu za afya kupitia page yangu iitwayo Gurti health consultant.
Kipindi cha nyuma alikuwa analalamikiwa mama kwa kuzaa watoto wa kike tupu au wakiume tupu pasipo kujua anayeamua jinsia ya mtoto ni mwanaume nashukuru Mungu sasa hivi jamii imeanza kutambua hilo
MTOTO WA KIUME AU WA KIKE ANATOKEAJE?
Katika urutubishaji yai la mwanamke linabeba chromosome X yani XX
Na mbegu ya mwanaume inabeba chromosome XY
Chromosome X kutoka kwa mwanamke ikikutana na Y kutoka kwa mwanaume mtoto wa kiume hupatikana
Chromosome X kutoka kwa mwanamke ikikutana na X kutoka kwa mwanaume mtoto wa kike hupatikana
FAHAMU SIFA ZA CHROMOSOMES X na Y za mwanaume
Ili uweze kufanikiwa kuchagua mtoto wa kiume au wa kike lazima ujue sifa za chromosomes hizi zinazoamua jinsia ya mtoto
SIFA ZA CHROMOSOMES Y
1.Zina spidi kubwa sana kwahiyo kama yai lipo tayari zenyewe zitawahi kwenda kurutubisha
2.Zina maisha mafupi sana kulinganisha na X
SIFA ZA CHROMOSOMES X
1.Zina spidi ndogo sana
2.Zina maisha marefu kulinganisha na Y
Baada ya kujua sifa za chromosome ambazo ndo zinatusaidia kuamua jinsia twende moja kwa moja kwenye jinsi ya kupata mtoto wa jinsia unayotaka
MAMBO YA KUZINGATIA KATIKA KUAMUA JINSIA
1.Lazima mwanamke ajue mzunguko wake (menstrual cycle)siku ya 1-28
2.Lazima mzunguko wako uwe na mpangilio sahihi(unaweza ukachunguza mzunguko wako kwa miezi minne mfululizo)
3.PH ya uke lazima iwe kiwango sahihi 4-5.5(Tumia neplily pad kwa kuwa na PH sahihi
4.Ushirikiano kati ya mwanamke na mwanaume
JINSI YA KUPATA MTOTO WA KIUME
Ili uweze kupata mtoto wa kiume kisayansi unashauriwa kushiriki tendo la ndoa siku ambayo yai litakuwa limetoka kama mzunguko wako uko sahihi ni siku ya 14
Njia nyingine ya kujua yai limetoka baba anaingiza vidole viwili ukeni wakati wa asubuhi na ukikuta uteute ujue yai limetoka kwahiyo jioni mnashiriki tendo la ndoa kwa ajili ya kupata mtoto wa kiume
KWANINI USHIRIKI TENDO LA NDOA WAKATI YAI LIMETOKA ILI KUPATA MTOTO WA KIUME?
Kisayansi chromosome Y ambayo inahusika katika kutunga mimba ya mtoto wa kiume ina spidi kubwa sana ni nyepesi na haiwezi kisihi mda mrefu kwahiyo ukishiriki tendo la ndoa wakati yai limetoka maana ake unaongeza nafasi ya kupata mtoto wa kiume
JINSI YA KUPATA MTOTO WA KIKE
Ili ufanikiwe kupata mtoto wa kike utatakiwa ushiriki tendo la ndoa siku tatu kabla ya yai kupevuka yani hapa ni baada ya kujua mzunguko
KWANINI USHIRIKI TENDO LA NDOA SIKU TATU KABLA
Hii ni kwasababu chromosome X ambazo ndo zinaunda mtoto wa kike huwa zina sifa ya kuwa na maisha marefu na kutembea taratibu hivyo yai likitolewa litakuta chromosome X ziko hai
KUNA BAADHI YA WAZEE WA ZAMANI WANAAMINI HAYA KATIKA KUPATA MTOTO WA JINSIA UNAYOTAKA
KUPATA WA KIKE
Kula samaki ,mboga za majani,matunda,bidhaa za maziwa,mbegu za matikiti majia na alzeti nk
Wakati wa kufanya tendo la ndoa mwanamke akae juu nk
KUPATA WA KIUME
Kula nyama, ndizi ,Vyakula vya chumvi kama chips ila usizidishe chumvi,karanga na vyakula vingine vya potassium na sodium
Chromosomes Y zinahitaji pH ya alkane kuliko asidi ndio maana wazee waliona hili
Kuna mengi kuhusu wazee wa zamani ila nmeongelea haya ya mlo kwa maana yana mantiki kibaiolojia
MAMBO YANAYOWEZA ATHIRI KUPATA MTOTO UNAYEMTAKA
1.Kushindwa kuhesabu siku( tumia chart niliyokuwekea)
2.Mzunguko mbovu wa hedhi(Tumia neplily pad)
3.Kutokuwa na PH sahihi ukeni tumia Neplily
Jumanne, 26 Julai 2016
Riek Machar ''apinduliwa'' Sudan Kusini
Nduguye Obama kumpigia kura Donald Trump
- Sikiliza: Sababu ya nduguye Obama kumuunga mkono Trump
- Barua za babake Obama zafichuliwa
- Mkewe Obama amtambua mbunifu kutoka Kenya
Jumamosi, 16 Julai 2016
Wanajeshi waasi 104 wauawa Uturuki
SOMA ZAIDI HAPA
-
Shule 10 zilizofanya vizuri: 1.Kisimiri,-Arusha 2.Feza Boys,-Dar es Salaam 3.Alliance Girls,-Mwanza 4. Feza Girls,-Dar es Salaam 5. Ma...
-
Image copyright PA WIRE Image caption George Osborne Waziri wa fedha wa Uingereza George Osborne ameeleza mipango ya wizara yake ...
-
Image copyright EPA Image caption Ethiopia imezima mitandao ya kijamii Mitandao ya kijamii nchini Ethiopia imezimwa. Waethiopia...
-
Image copyright GETTY Image caption Kiongozi wa mtandao wa kigaidi wa al Qaeda Osama bin Laden Mwanaye aliyekuwa kiongozi wa mtan...
-
Image copyright REUTERS Image caption Ndege zatumika katika mapigano Sudan Kusini Uganda imetangaza kwamba itatuma wanajeshi wake...
-
Image copyright GETTY Image caption Kane kupatiwa mkataba mnono Mshambuliaji wa England na Tottenham, Harry Kane atasaini mkataba mpy...
-
Discuss the merits and demerits of nucleated (or dispersed) settlements for agricultural development in Tanzania. Note 1: work in groups...