Jumatatu, 11 Julai 2016

Mashabiki Ureno waendelea kusherehekea


Image copyrightAFP
Image captionHii ni mara ya kwanza kwa Ureno kushinda taji kubwa kama hilo.
Kundi kubwa la mashabiki wa Ureno limeendelea kusheherekea bada ya timu yao ya taifa kuifunga Ufaransa katika michuano ya Euro 2016 mjini Paris.
Ureno imeshinda 1-0 katika muda wa nyongeza na kuwaacha mashabiki wa Ufaransa katika hali ya simanzi ndani ya dimba la Stade de France huku mitaa ya Lisbon ikirindima kwa shangwe kubwa.
Ureno illicheka karibia mda wote bila huduma ya nyota wake Cristiano Ronaldo aliyeumia na kutolewa nje dakika 25 ya mchezo huo na baadaye kurejea na kulinyanyua kombe hilo.
Amesema kombe hilo ni kwa ajili ya Wareno wote pamoja na wote wanaioshabikia timu hiyo mjini Paris.
Hii ni mara ya kwanza kwa Ureno kushinda taji kubwa kama hilo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

SOMA ZAIDI HAPA