BREAKING NEWS

Jumatatu, 5 Septemba 2016

Majina mashuhuri zaidi ya watoto


 Mtoto
TJina Noah limeingia kwenye orodha ya majina 10 mashuhuri zaidi kwa kupewa watoto wavulana kwa mara ya kwanza, huku Amelia likisalia kuwa jina ambalo wazazi wengi wanawapa watoto wasichana England na Wales, taasisi ya taifa ya Takwimu Uingereza imeonesha.
Jina Oliver ndio linaloongoza upande wa wavulana, likishikilia nafasi ya kwanza tangu 2013 nalo Amelia likiwa juu kwa wasichana tangu 2011. Watoto walioitwa Oliver mwaka 2015 ni 6,941 na Amelia 5,158.
Maafisa wa ONS waliorodhesha majina kando kwa mujibu wa jinsi jina liliandikwa.
Iwapo majina yanayotamwa kwa njia sawa yangewekwa pamoja, basi orodha hiyo huenda ingelikuwa tofauti kidogo.
Mfano ni jina Muhammad ambalo linashikilia nafasi ya 12 likiwa na watoto 3,730.
Kuna wazazi walioandika jina hilo kama Mohammed (2,332) na wengine kama Mohammad (976). Iwapo majina hayo yangejumlishwa, basi jina hilo lingelikuwa katika 10 bora.
Yalikuwepo majina ya kushangaza. Kwa mfano watoto wavulana 17 na wasichana 15 walipewa jina Baby.
Majuzi, utafiti ulionesha karibu sehemu moja kati ya tano ya wazazi Uingereza wanajutia majina waliyowapa watoto wao.
Image copyright Alamy
Image caption Rocky Balboa na Apollo Creed
Wavulana 35 walipewa jina Rocky, na 21 wakapewa Apollo, labda kutokana na wahusika wakuu wa filamu ya ndondi Rocky Balboa na Apollo Creed.
Wavulana 15 walipewa jina Blue na wengine 14 wakaitwa Ocean. Na kunao 18 walipewa jina Blu.
Kuna jumla ya wavulana 36 ambao watahitajika kujifunza kuandika na kutamka jina lao, Tymoteusz.
Image copyright PA
Image caption Wasichana watano wameitwa Kaleesi
Upande wa wasichana 280 walipewa jina Arya, mmoja wa wahusika wakuu filamu ya Game of Thrones, na wengine 562 wakaitwa Aria, 33 Ariah, 17 Aaria na sita Aariah, jina ambalo huenda ni moja ila likaandikwa tofauti.
Jina Kaleesi, pia kutoka kwa filamu hiyo, lilipewa wasichana watano.
Jina Princess lilipewa wasichana 72, ikikaribia wavulana 77 walioitwa Prince.
Image copyright Alamy
Image caption Perhaps boys called Maverick will grow up to become a Top Gun in whatever they do
Takwimu hizo zinaonesha jina Oliver ndilo maarufu zaidi kwa wavulana maeneo yoteb ya Englandisipokuwa London na West Midlands, ambapo jina Muhammad linaongoza.
Jina Muhammad lilipita Oliver eneo la West Midlands mwaka 2014.

Majina mashuhuri zaidi 2015
Image caption Jina la marehemu Oliver Reed linasalia kuwa maarufu zaidi kupewa wavulana
  • Oliver 6,941
  • Jack 5,371
  • Harry 5,308
  • George 4,869
  • Jacob 4,850
  • Charlie 4,831
  • Noah 4,148
  • William 4,083
  • Thomas 4,075
  • Oscar 4,066

Majina maarufu kwa wasichana 2015
Image copyright EPA
Image caption Amelia Boynton Robinson, mwanaharakati mtetezi wa haki za raia Marekani, alifariki mwaka jana akiwa na umri wa miaka 104
  • Amelia 5,158
  • Olivia 4,853
  • Emily 3,893
  • Isla 3,474
  • Ava 3,414
  • Ella 3,028
  • Jessica 2,937
  • Isabella 2,876
  • Mia 2,842
  • Poppy 2,816

Image copyright Reuters
Image caption Wasichana kadha pia wamepewa jina la mwanamuziki Rihanna
Wasichana 72 walipewa jina Adele, 39 wakaitwa Paloma, kutokana na mwanamuziki Paloma Faith.
Kulikuwa na wasichana 35 walioitwa Rihanna, na tisa Rhianna.
Majina 50 mashuhuri zaidi ya wavulana na wasichana England na Wales mwaka 2015
Wavulana Wasichana






Nambari Jina Watoto Nambari Jina Watoto






1 OLIVER 6941 1 AMELIA 5158
2 JACK 5371 2 OLIVIA 4853
3 HARRY 5308 3 EMILY 3893
4 GEORGE 4869 4 ISLA 3474
5 JACOB 4850 5 AVA 3414
6 CHARLIE 4831 6 ELLA 3028
7 NOAH 4148 7 JESSICA 2937
8 WILLIAM 4083 8 ISABELLA 2876
9 THOMAS 4075 9 MIA 2842
10 OSCAR 4066 10 POPPY 2816
11 JAMES 3912 11 SOPHIE 2779
12 MUHAMMAD 3730 12 SOPHIA 2744
13 HENRY 3581 13 LILY 2711
14 ALFIE 3540 14 GRACE 2658
15 LEO 3468 15 EVIE 2529
16 JOSHUA 3394 16 SCARLETT 2285
17 FREDDIE 3219 17 RUBY 2215
18 ETHAN 2940 18 CHLOE 2158
19 ARCHIE 2912 19 ISABELLE 2119
20 ISAAC 2829 20 DAISY 2113
21 JOSEPH 2786 21 FREYA 2090
22 ALEXANDER 2759 22 PHOEBE 2081
23 SAMUEL 2705 23 FLORENCE 2053
24 DANIEL 2622 24 ALICE 2006
25 LOGAN 2610 25 CHARLOTTE 1951
26 EDWARD 2593 26 SIENNA 1941
27 LUCAS 2448 27 MATILDA 1774
28 MAX 2407 28 EVELYN 1770
29 MOHAMMED 2332 29 EVA 1753
30 BENJAMIN 2328 30 MILLIE 1673
31 MASON 2263 31 SOFIA 1640
32 HARRISON 2241 32 LUCY 1525
33 THEO 2103 33 ELSIE 1513
34 JAKE 2013 34 IMOGEN 1478
35 SEBASTIAN 1988 35 LAYLA 1428
36 FINLEY 1978 36 ROSIE 1403
37 ARTHUR 1966 37 MAYA 1354
38 ADAM 1903 38 ESME 1340
38 DYLAN 1903 39 ELIZABETH 1338
40 RILEY 1728 40 LOLA 1322
41 ZACHARY 1644 41 WILLOW 1308
42 TEDDY 1430 42 IVY 1275
43 DAVID 1394 43 ERIN 1249
44 TOBY 1363 44 HOLLY 1248
45 THEODORE 1302 45 EMILIA 1243
46 ELIJAH 1294 46 MOLLY 1215
47 MATTHEW 1279 47 ELLIE 1185
48 JENSON 1223 48 JASMINE 1182
49 JAYDEN 1219 49 ELIZA 1171
50 HARVEY 1190 50 LILLY 1146

Kiir akubali wanajeshi wa UN watumwe Juba, Sudan Kusini

Wanajeshi wa UN

Wanajeshi hao wapya watatoka Ethiopia, Kenya, Rwanda, Sudan na Uganda
Rais wa Sudan Kusini hatimaye amekubali kikosi cha ziada cha wanajeshi wa kulinda amani kitumwe nchini humo.
Rais Salva Kiir alichukua hatua hiyo baada ya kufanya mazungumzo na ujumbe kutoka kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Bw Kiir alikuwa awali amekataa kutumwa kwa wanajeshi hao 4,000 kutoka mataifa ya kanda, akisema huo ni ukiukaji wa uhuru wa Sudan Kusini.
UN iliidhinisha kutumwa kwa wanajeshi hao baada ya kuzuka upya kwa vita baina ya wanajeshi waaminifu kwa Bw Kiir na aliyekuwa makamu wake wa rais Dkt Riek Machar mwezi Julai mjini Juba.
Kikosi hicho cha ziada kitakuwa na mamlaka zaidi kushinda kikosi cha sasa cha wanajeshi 13,000 ambacho kimekuwa kikihudumu nchini humo

SOMA ZAIDI HAPA