BREAKING NEWS

Alhamisi, 5 Januari 2017

Trump kuondoa sheria ya afya ya Obamacare Marekani



Kuondoa sheria hiyo ilikuwa moja ya vipaumbele vya Trump alipokuwa akiwania urais
Image captionKuondoa sheria hiyo ilikuwa moja ya vipaumbele vya Trump alipokuwa akiwania urais
Makamu wa Rais mteule wa Marekani Mike Pence amesema mchakato wa kufutilia mbali sheria ya afya iliyoanzishwa na Obama utaanza siku ya kwanza Donald Trump atakapoingia madarakani.
Baada ya mkutano na wanachama wa Republican na viongozi katika bunge la congress,Pence amesema Rais mteule alikuwa anashughulikia sheria mahususi zinazohusika ili kuruhusu mabadiliko kuelekea katika mfumo mpya wa sheria za afya.
Lakini amesema mbivu na mbichi zitajulikana baada ya miezi kadhaa.
Msemaji wa serikali Paul Ryan amesema atahakikisha kwamba hapatakuwapo mtu yeyete atakayewaangusha.
Makamu wa Rais mteule wa Marekani Mike Pence
Image captionMakamu wa Rais mteule wa Marekani Mike Pence
Bw Trump amesema kwamba wanachama wa Republican wanatakiwa kuhakikisha kwamba wanachama wa Democratic wanalaumiwa kwa kile alichokitaja kama 'Maafa ya sheria ya afya yaliyoanzishwa na Barack Obama'.
Lakini kiongozi wa chama cha Deomocratic katika bunge la senati Chuck Schumer amesema chochote kilichotokea ni jukumu la Republican jambo ambalo ni wazi na rahisi.

SOMA ZAIDI HAPA