BREAKING NEWS

Jumamosi, 11 Juni 2016

KIJANA WA KINEPAL APATA UGONJWA WA KUGEUKA JIWE.

Kijana wa miaka 11 apata ugonjwa wa kugeuka jiwe.
Ramesh kumari kutoka Nepal mwenye umri wa miaka 11 anaugua ugonjwa wa uso na mwili kugeuka jiwe.

Babake Nanda anasema ugonjwa huu ulianza akiwa na siku 15 baada ya kuzaliwa.
Anasema ngozi yake alianza kuwa nyeusi na kuwa ngumu.

Mwimbaji Joss Stones amelipia ada za matibabu ya mtoto huyu kwa ajili ya upasuaji.
Kulingana na madktari Ramesh ana aina fulani ya saratani ya ngozi.

Jumatano, 8 Juni 2016

Nyani azima umeme kote nchini Kenya

Kampuni ya kuzalisha umeme nchini Kenya, KENGEN imetuma taarifa kwa vyombo vya habari ikiomba radhi kwa ukosefu wa umeme Kwa hapo jana.
Hilo sio jambo geni.
Mara kwa mara umeme hupotea nchini Kenya kwa sababu moja au nyengine, sawa tu na mataifa yote barani Afrika
Hata hivyo sababu walioitoa KENGEN kwa ukosefu huo wa umeme Kwa takriban saa nne kote nchini humo ndio imewaacha wengi wamepigwa na butwaa !
Nyani.

 

Amini usiamini, KENGEN imempata nyani mmoja katika eneo maalum lenye 'swichi' hiyo katika mtambo wa kuzalisha umeme ulioko kwenye bwawa kuu la Gitaru Mashariki mwa Kenya.
Sasa kampuni hiyo inasema huenda nyani huyo ndiye aliyezima umeme kote nchini Kenya !
Kengen inasema kuwa huenda nyani huyo aliangukia mashine hiyo ndogo na ''kusababisha hitilafu ya takriban megawati 180 za umeme ambao ndio uliosababisha ukosefu wa umeme kote nchini Kenya.''
Kwa takriban saa nne taarifa hiyo ilielezea.

SOMA ZAIDI HAPA