BREAKING NEWS

Ijumaa, 20 Mei 2016

Msichana wa Chibok akutana na Buhari


Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari amekutana na msichana wa Chibok aliyeokolewa Amina Ali Nkeki, mtoto wake msichana wa miezi minne na mamake katika ikulu ya rais mjini Abuja.
Rais Buhari amesema kuwa ni furaha kubwa kuwa Amina amepata uhuru wake na kuongeza kuwa serikali yake itafanya kila iwezalo kuhakikisha kuwa ameishi maisha mazuri.
Aidha amesema kuwa pia litakuwa jukumu la serikali kuhakikisha kuwa ameendelea na masomo yake.
Amina aliokolewa kutoka mikononi mwa wanamgambo wa Boko Haram siku ya Jumatano, baada ya kuzuiliwa na wanamgambo hao kwa zaidi ya miaka miwili.
Yeye ni miongoni mwa wasichana zaidi ya mia mbili wa shule ambao walitekwa kutoka shule yao mjini Chibok na ndiye wa kwanza kuokolewa.

SOMA ZAIDI HAPA