Maandamano yalianza Burundi Aprili mwaka jana
Mahakama ya rufaa nchini Burundi imewahukumu washtakiwa 21 vifungo vya maisha jela baada ya kuwapata na hatia ya kushiriki jaribio la mapinduzi mwaka jana.
Washtakiwa hao ni kati ya 28 waliokuwa wameshtakiwa kuhusiana na jaribio hilo la Mei mwaka jana ambalo halikufaulu.
Miongoni mwao ni watano ambao walikuwa wamepatikana bila hatia na mahakama ya kwanza.
Mahakama hiyo ya rufaa imeagiza wakamatwe.
Upande wa mashtaka ulikata rufaa dhidi ya hukumu iliyotolewa na mahakama ya chini ukisema hukumu hiyo haikuwa kali vya kutosha.
UN: Watu 474 wameuawa Burundi
Mataifa ya Kifaransa yavunja uhusiano wao na Burundi
Wale waliopatikana na hatia pia wametakiwa kulipa zaidi ya $3.5m (£2.4m) kama fidia kutokana na vifo na uharibifu wa mali uliotokea wakati wa jaribio hilo la kupindua serikali.
Baadhi ya majenerali kwenye jeshi na baadi ya maafisa wakuu katika idara ya polisi walijaribu kumpindua Rais Pierre Nkurunziza baada yake kuamua kuwania urais kwa muhula wa tatu.
Uamuzi wa leo unatazamwa kama ushindi wa serikali ambayo imekuwa ikijaribu kujenga uhusiano wa moja kwa moja baina ya jaribio hilo la mapinduzi na maandamano ya kupinga hatua ya Rais Nkurunziza kuwania kwa muhula wa tatu.
Maandamano hayo yalianza wiki mbili kabla ya mapinduzi.
BREAKING NEWS
-
Nucleated rural settlement Advantages More interaction with people. Safer as there are more people. Can share ideas on how to solve a p...
Jumatatu, 9 Mei 2016
Washtakiwa 21 wafungwa jela maisha Burundi
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
SOMA ZAIDI HAPA
-
Nucleated rural settlement Advantages More interaction with people. Safer as there are more people. Can share ideas on how to solve a p...
-
MMOJA wa madereva waliosababisha ajali ya mabasi ya City Boy Jumatatu iliyopita katika kijiji cha Maweni wilayani Manyoni, Jeremiah Semfu...
-
Kilimo cha miti kimepata umaarufu wa ghafla miaka ya hivi karibuni kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ongezeko la mahitaji ya mazao ya m...
-
Image copyright EPA Wafungwa watatu wameuawa wakati wa maandamano kwenye gereza moja lililo kusini mwa Thailand. Karibu wafungw...
-
Image copyright NASA Image caption Satelite ya Juno kama inavyoonekana Ile Setilaiti ya Juno iliiyosafiri kwa miaka mitano kwenda kat...
-
Kijana wa miaka 11 apata ugonjwa wa kugeuka jiwe. Ramesh kumari kutoka Nepal mwenye umri wa miaka 11 anaugua ugonjwa wa uso na mwili kugeuk...
-
DIRA TV: Hujambo, Je, kama mzazi, ni mbinu zipi unaweza kutumia kuhakikisha mtoto wako wa kike/binti anamaliza masomo yake bila kupata vis...
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni