WATU wawili wanaosadikika kuwa ni majambazi ambao wametokea Njombe wameuwawa katika majibizano ya risasi na polisi baada ya kuvamia Pub ya Mama Siyovelwa iliyopo eneo la mtaa wa Ikulu mjini Iringa
Tukio hilo limetokea majira ya saa 10:45 jioni ya jana tarehe 30/04/2016 baada ya watu hao kuvamia Pub hiyo kwa lengo la kupora kabla ya raia wema kutoa taarifa polisi
Baadhi ya mashuhuda waliokuwepo eneo hilo wamesema kuwa watu hao walihofiwa mapema wakati wa kuingia eneo hilo ambapo inadaiwa walikuwa watatu na mmoja alijichanganya na Raia na kujificha.
Kazi kubwa iliyofanywa na polisi imefanikisha watu hao wawili waliokuwa na silaha kuuwawa bila raia wengine kujeruhiwa
Miili miwili ya watu hao wanaosadikika ni majambazi ambao baada ya kupekuliwa wamekutwa na tiketi za basi la Hapy National kutoka Njombe imepelekwa hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa
Taarifa zaidi utazidi kuzipata japo Njombe kuna mauwaji ya kutumia silaha ambayo yalitokea juzi
Jumamosi, 30 Aprili 2016
MAJAMBAZI WAWILI WAUAWA IRINGA
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
SOMA ZAIDI HAPA
-
Shule 10 zilizofanya vizuri: 1.Kisimiri,-Arusha 2.Feza Boys,-Dar es Salaam 3.Alliance Girls,-Mwanza 4. Feza Girls,-Dar es Salaam 5. Ma...
-
Im Madaktari nchini India wamepandikiza pua mpya katika uso wa mvulana wa miaka 12 iliokuwa imemea katika paa lake la uso. Pua ...
-
Mwanamume mmoja katika mji wa Bungoma, Magharibi mwa Kenya ameshangaza wengi baada...
-
. Na; Martin Maranja Masese. Vijana ndiyo nguvu kazi ya Taifa lolote lenye maendeleo katika Dunia hii.. lakini asilimia kubwa ya vijana hi...
-
Image copyright Image capti Mwanafunzi mmoja wa chuo kikuu kimoja nchini Kenya amejitia kitanzi baada ya kupoteza dau la shilingi...
-
N MKOA NAMBA YA SHULE JINA LA SHULE JINSI JINA 1 GEITA S1164 MISSUNGWI SECONDARY SCHOOL F ...
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni