Jumanne, 5 Julai 2016

Setilaiti ya Juno yafika Jupiter



Image copyrightNASA
Image captionSatelite ya Juno kama inavyoonekana
Ile Setilaiti ya Juno iliiyosafiri kwa miaka mitano kwenda katika sayari ya Jupiter imefika kwenye sayari hiyo na kuanza kuizunguka.
Wanasayansi wanakadiria setilaiti hiyo ilifika muda mfupi ujao majira ya saa 12:15 asubuhi hii kwa saa za Afrika Mashariki.
Setilaiti hiyo inatarajiwa kudumu kwa mwaka mmoja na nusu kuchunguza sayari jinsi ilivyoumbwa.
Mawasiliano kutoka kwa chombo hicho cha juu yalipokelewa katika maabara ya Nasa eneo la Pasadena, California kwa shangwe.
"Vituo vyote vya Juno, tunapokea sauti ya kufanikiwa kwa chombo Delta B," kituo cha udhibiti wa Juno kilitangaza. "Roger Juno, karibu Jupiter."
JunoImage copyrightGETTY
Image captionChombo cha Juno kikipaa
Wanasayansi wanatarajiwa kutumia chombo hicho kufahamu Zaidi muundo wa sayari ya Jupiter ambayo hujulikana kwa Kiswahili kama Zohali.
Wanafikiri muundo wake kikemia unaweza kutoa ufahamu kuhusu jinsi sayari hiyo iliundwa miaka bilioni nne unusu iliyopita.
Hakuna chombo cha anga za juu kilichowahi kufika karibu sana na sayari hiyo kama kilivyofanya chombo cha Juno.
Miali nururishi kutoka kwa sayari hiyo huwa na uwezo wa kuharibu vyombo vya kielektroniki visivyokingwa vyema.
Chombo vya Juno kimezingirwa na kinga ya madini ya Titanium.
Kwa sasa Juno itakuwa ikichukua siku 53 kuizunguka sayari hiyo.
Baadaye Oktoba, itaongeza kasi na kuikaribia zaidi sayari hiyo na kuanza kutumia siku 14 kumaliza mzunguko.
Image copyrightGETTY
Lengo kuu litakuwa kubaini iwapo kuna oksijeni katika sayari hiyo. Hii sana itakuwa imefungamanishwa na maji, iwapo yapo.
"Kiwango cha maji katika sayari ya Jupiter kitatueleza mengi kuhusu ni wapo sayari hiyo ilikuwa ilipoundwa mapema katika mfumo wa jua,” anasema mmoja wa wanasayansi wanaohusika katika mradi huo Candy Hansen.
"Tunafikiri kwamba Jupiter iliundwa ikiwa pahala tofauti na ilipo sasa."
  • Jupiter ina ukubwa mara 11 kuzidi Dunia na uzito wake ni mara 300 zaidi
  • Sayari hiyo hutumia miaka 12 ya dunia kulizunguka jua; siku moja huko hudumu saa 10.
  • Muundo wake ni kama wa nyota , sana haidrojeni na helium.
Nasa inapanga kuitumia Juno hadi Februari 2018.
Image copyrigh

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

SOMA ZAIDI HAPA