Jumamosi, 16 Julai 2016

Mamia wapigwa picha wakiwa utupu Uingereza


Alfred GelderImage copyrightAFP
Image captionBarabara ya Alfred Gelder iligeuzwa kuwa bahari ya watu
Watu zaidi ya 3,000 walipigwa picha wakiwa utupu nchini Uingereza chini ya mradi wa kuadhimisha na kusherehekea utamaduni.
Mradi huo uliopewa jina Bahari ya Hull unatumiwa kusherehekea mji wa Hull kama Mji wa Utamaduni kwenye sherehe kuu mwaka ujao.
Baraza la Jiji la Hull lilisema mradi huo wa sanaa, ndio mkubwa zaidi wa aina yake kufanyika Uingereza.
Image copyrightAFP
Uliendeshwa na mpigapicha mashuhuri duniani Spencer Tunick na kushirikisha watu 3,200 kutoka nchi 20, ambao walipigwa picha katika maeneo mbalimbali maarufu mjini humo Jumamosi iliyopita.
WalioshirikiImage copyrightREUTERS
Image captionWatu wa kujitolea kutoka nchi 20 walishiriki
Picha hizo, ambazo zinasimamiwa na shirika la maonesho ya Sanaa la Ferens Art Gallery, zitawekwa kwenye maonesho wakati wa shughuli za Jiji la Utamaduni Uingereza mwaka 2017.
Maelfu ya watu walifika kabla ya jua kuchomoza na wakapakwa rangi ya samawati iliyokozwa kwa viwango vinne, kuashiria maji.

Walipigiwa picha maeneo mbalimbali yakiwemo Bustani ya Malkia, Guildhall na daraja la Scale Lane.
Shughuli yote ilidumu saa nne.
Image copyrightAP
Mmoja wa walioshiriki alikuwa Stephane Janssen, mwenye umri wa miaka 80 anayetoka Brussels.
Ameshiriki miradi ya upigaji picha wa watu wengi wakiwa utupu ya Tunick mara 20 awali.
TunickImage copyrightPA
Image captionBw Tunick (kushoto) akiwa na Janssen
“Ni maridadi sana, ni kupakwa rangi kidogo tu. Kila mtu ni sawa – hakuna tofauti ya rangi au jinsia – kila mtu ni sawa na yule mwingine akiwa utupu, na hilo ndilo napenda,” alisema.
Sarah Hossack, kutoka Hull, alisema alifurahia sana.
Image copyrightAFP
“Nilikuwa utupu tangu saa kumi alfajiri. Lakini nilifurahia sana. Shughuli hiyo ilituleta pamoja,” alisema.
Mradi huo wa Hull uliushinda ule wa Gateshead wa mwaka 2005 ambapo ni watu 1,700 waliojitokeza pamoja na ule wa Salford wa mwaka 2010 ambapo watu 1,000 walishiriki.
Image copyrightAFP
Kirsten Simister, afisa katika Ferens Art Gallery, alisema alishangazwa sana na idadi ya watu waliojitokeza Hull.
Tunick, ambaye makao yake ni New York, amefanya miradi mingine 90 kama huo wa Hull.
Amewahi kupigia watu wengi kwa pamoja picha katika Sydney Opera House, Place des Arts mjini Montreal, Mexico City na Munich nchini Ujerumani.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

SOMA ZAIDI HAPA