Alhamisi, 12 Mei 2016

Wanasayansi waunda ngozi kuziba uzee



Wanasayansi wanadai kuunda aina ya ngozi inayoweza kubandikwa juu ya mwili wa mtu kupunguza muonekano wa mikunjo ya ngozi mwilini na ngozi inayopwaya chini ya macho kutokana na uzee.Ni aina ya maji maji mtu anayopaka mwilini alafu inaachwa kukauka ambapo baadaye husihia kuwa ngozi nyembamba iliyo mithili ya 'ngozi ya ujana, Nature Materials inaarifu baada ya kufanya majiribio kadhaa madogo.
Kwa sasa inafanyiwa majaribio ya kuuzwa kama bidhaa ya urembo.
Lakini wanasayansi Marekani wanasema "ngozi ya pili " huenda baadaye ikaweza kutumika kutengeneza dawa na kinga dhdi ya jua.
Ngozi ya piliKundi la wanasayansi kutoka chuo kikuu cha Havard kitengo cha matibabu na taasisi ya teknolojia Massachusetts wamefanya majaribio ya bidhaa hiyo kwa watu waliojitolea ambao walipakwa ngozi hiyo chini ya macho, kwenye mikoni yao na miguu.
Ngozi hiyo inayotokana na kemikali polysiloxane polymer iliundwa kwenye maabara kwa kutumia chembe chembe za Silicone na hewa safi ya Oxygen.
Licha ya kwamba sio ngozi ya kweli lakini imeundwa kuiga ngozi asili na pia kuacha nafasi ya hewa kupita.
Kwa mujibu wa watatfiti ngozi hiyo bandia ina uwezo wa kunasa mvuke na kusaidia ngozi kujivuta kiasi cha inavyostahili.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

SOMA ZAIDI HAPA