Alhamisi, 12 Mei 2016

Polisi waandamana dhidi ya Beyonce




Kundi moja la maafisa wa polisi limefanya maandamano karibu na tamasha lililofanyika katika mji wa nyumbani wa nyota wa muziki Beyonce huko Houston.
Wanachama wa muungano wa polisi na Sherrif walisimama mbali na uwanja wa soka na kuelekeza mwangaza wa bluu katika ukumbi wa tamasha hilo.
Walikuwa wanapinga kanda ya video ya Beyonce ambayo wanasema inawaponza polisi.
 

Mwanamuziki huyo tayari amesema kwamba hawakosoi polisi katika wimbo huo na kusema kuwa maafisa wa polisi wanaodhani aliwaponza wanakosea.
Mwanachama mmoja wa polisi amekiambia chombo cha habari KHOU11 kwamba hawakufurahia baada ya Beyonce kutumia picha za gari moja la polisi mjini New Orleans iliokuwa ikizama katikamafuriko.
''Tunaamini kwamba baadhi ya mambo yake ni kinyume na maafisa wa polisi'',alisema.

Mnamo mwezi Aprili,Beyonce aliambia jarida la Elle kwamba anaheshimu polisi lakini hapendi unyanyasaji.
''Mtu yoyote anyedhani kwamba siwapendi polisi anakosa kwa sababu'', alisema.
''Ninawapenda na kuwaheshimu sana polisi pamoja na familia za maafisa hao ambao hujitolea ili kuhakikisha tuko salama''.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

SOMA ZAIDI HAPA